Loading...

UONGOZI INSTITUTE WAFANYA KONGAMANO LA KUKUZA, KUIMARISHA UONGOZI NA VIONGOZI NCHINI

Loading...
UONGOZI INSTITUTE WAFANYA KONGAMANO LA KUKUZA, KUIMARISHA UONGOZI NA VIONGOZI NCHINI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa UONGOZI INSTITUTE WAFANYA KONGAMANO LA KUKUZA, KUIMARISHA UONGOZI NA VIONGOZI NCHINI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : UONGOZI INSTITUTE WAFANYA KONGAMANO LA KUKUZA, KUIMARISHA UONGOZI NA VIONGOZI NCHINI
link : UONGOZI INSTITUTE WAFANYA KONGAMANO LA KUKUZA, KUIMARISHA UONGOZI NA VIONGOZI NCHINI

soma pia


UONGOZI INSTITUTE WAFANYA KONGAMANO LA KUKUZA, KUIMARISHA UONGOZI NA VIONGOZI NCHINI

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii.

TAASISI ya Uongozi nchini (Uongozi Institute) imefanya kongamano lenye mlengo wa kukuza na kuimarisha uongozi na viongozi nchini hasa katika kutekeleza majukumu yao katika sekta wanazohudumia.

Akimwakilisha  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora George Mkuchika wakati  wa uzinduzi wa kongamano hilo  mjumbe wa bodi ya Taasisi ya Uongozi Prof. Penina Mlama amesema kuwa lengo la kufanya kongamano hilo ni  kubadilishana mawazo kuhusu kukuza na kuimarisha masuala ya uongozi na viongozi nchini hasa katika utendaji.

Ameeleza kuwa mawazo yatakayotolewa katika mjadala huo yatumike katika kuboresha uongozi serikalini na katika sekta binafsi na yaendelezwe ili kuwawezesha viongozi kutenda kazi kwa kuzingatia misingi bora zaidi.Aidha ameeleza  Serikali iliona tatizo katika masuala ya uongozi na ilipofika mwaka 2010 Serikali ilianzisha Taasisi ya Uongozi (Uongozi Institute) ili kuwajengea uwezo na kuwaimarisha katika utekelezaji wao wa majukumu.

Mlama amesema kuwa Serikali ya Awamu tano imedhamiria katika kuhakikisha viongozi wanafanya kazi kwa kuzingatia mihimili na maadili kwa ujumla na amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais Dk. John Magufuli amesimamia kwa kiasi kikubwa masuala ya uadilifu, nidhamu katika matumizi ya fedha za umma, maadili sehemu za kazi na kupiga vita vitendo vya rushwa na ufisadi.

Kwa upande wake  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Prof. Joseph Semboja amesema kuwa kongamano hilo ni la kubadilishana mawazo kuhusiana na ukuzaji na uimarishaji wa uongozi na viongozi nchini na washiriki wametoka katika sekta mbalimbali ikiwemo Serikalini, Bungeni, Jeshini, vyama vya siasa na dini.Semboja amesema kuwa kongamano hilo ni la kupanga mikakati na sio kutathimini mifumo iliyopita na ya sasa. Na ameeleza kuwa watatathimini mifumo ili kujenga matokeo bora hapo baadaye.

Amesema kuwa historia inaonesha kuwa viongozi wanaofanya vizuri wanajengwa kutokana na mazingira ambayo watakuja kuongoza na wao kama taasisi watahakikisha wanasimamia majukumu hayo kikamilifu kwa kuandaa mijadala na makongamano mbalimbali yanayolenga kukuza na kuimarisha masuala ya uongozi na viongozi nchini.
 Aliyekuwa Spika wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Anna Makinda (kushoto) na aliyekuwa Waziri wa fedha Zakia Meghji wakifuatilia mjadala huo uliokuwa ukiongozwa  prof. Issa Shivji.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Prof. Joseph Semboja akihutubia wakati wa kongamano hilo ambapo ameeleza kuwa Taasisi hiyo itaendelea kuandaa mijadala na mada mbalimbali katika kukuza na kuimarisha uongozi na viongozi nchini.
 Mjumbe wa bodi ya Taasisi ya Uongozi Prof. Penina Mlama akisoma hotuba wakati wa uzinduzi wa kongamano lililokuwa na mlengo wa kukuza na kuimarisha uongozi na viongozi nchini lililofanyika leo jijini Dar es salaam.
Aliyekuwa Spika wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Anna Makinda (kushoto) na aliyekuwa Waziri wa fedha Zakia Meghji wakifuatilia mjadala huo uliokuwa ukiongozwa  prof. Issa Shivji.


Hivyo makala UONGOZI INSTITUTE WAFANYA KONGAMANO LA KUKUZA, KUIMARISHA UONGOZI NA VIONGOZI NCHINI

yaani makala yote UONGOZI INSTITUTE WAFANYA KONGAMANO LA KUKUZA, KUIMARISHA UONGOZI NA VIONGOZI NCHINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala UONGOZI INSTITUTE WAFANYA KONGAMANO LA KUKUZA, KUIMARISHA UONGOZI NA VIONGOZI NCHINI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/uongozi-institute-wafanya-kongamano-la.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "UONGOZI INSTITUTE WAFANYA KONGAMANO LA KUKUZA, KUIMARISHA UONGOZI NA VIONGOZI NCHINI"

Post a Comment

Loading...