Loading...
title : USAFIRI WAKWAMISHA KUFIKISHWA MAHAKAMANI KWA SETHI NA RUGEMARILA
link : USAFIRI WAKWAMISHA KUFIKISHWA MAHAKAMANI KWA SETHI NA RUGEMARILA
USAFIRI WAKWAMISHA KUFIKISHWA MAHAKAMANI KWA SETHI NA RUGEMARILA
Na Karama Kenyunko Blogu ya Jamii.
UPANDE wa mashtaka katika kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili, washtakiwa Harbinder Sethi na James Rugemarila umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa, washtakiwa wameshindwa kufikishwa mahakamani hapo kwa sababu ya kuwepo kwa shida ya usafiri.
Wakili wa serikali Emmanuel Nitume ameeleza hayo Leo Novemba 22,2018 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.
"Mheshimiwa, kesi leo imekuja kwa ajili ya kutajwa, upelelezi bado haujakamilika na pia washtakiwa wote wanaokabiliwa na kesi hiyo hawapo kwa sababu kuna shida ya usafiri." Amesema Nitume.
Wakati wakili huyo wa serikali akieleza hayo, afisa mmoja wa Magereza aliyekuwemo mahakamani humo aliongeza kuiambia mahakama kuwa washtakiwa hawajaletwa kwa sababu kuna shida ya magari.
Kufuatia melezo hayo, Hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi Desemba 6, mwaka huu.
Katika kesi hiyo,Washtakiwa Sethi na Rugemalira wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi kwa kula njama, kujihusisha mtandao wa uhalifu , kughushi, kutoa nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu, kutakatisha fedha na kusababisha hasara ya USD 22, 198,544.60 na Sh 309,461,300,158.27.
Hivyo makala USAFIRI WAKWAMISHA KUFIKISHWA MAHAKAMANI KWA SETHI NA RUGEMARILA
yaani makala yote USAFIRI WAKWAMISHA KUFIKISHWA MAHAKAMANI KWA SETHI NA RUGEMARILA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala USAFIRI WAKWAMISHA KUFIKISHWA MAHAKAMANI KWA SETHI NA RUGEMARILA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/usafiri-wakwamisha-kufikishwa.html
0 Response to "USAFIRI WAKWAMISHA KUFIKISHWA MAHAKAMANI KWA SETHI NA RUGEMARILA"
Post a Comment