Loading...

WAZIRI LUGOLA AWAAMBIA MABALOZI NCHI IPO SALAMA, AAHIDI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NAO

Loading...
WAZIRI LUGOLA AWAAMBIA MABALOZI NCHI IPO SALAMA, AAHIDI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NAO - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI LUGOLA AWAAMBIA MABALOZI NCHI IPO SALAMA, AAHIDI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NAO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI LUGOLA AWAAMBIA MABALOZI NCHI IPO SALAMA, AAHIDI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NAO
link : WAZIRI LUGOLA AWAAMBIA MABALOZI NCHI IPO SALAMA, AAHIDI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NAO

soma pia


WAZIRI LUGOLA AWAAMBIA MABALOZI NCHI IPO SALAMA, AAHIDI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NAO



Na Felix Mwagara, MOHA.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amefanya mazungumzo na Balozi wa Italia, Kenya na Afrika Kusini katika ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam, na kuwaambia ulinzi na usalama wa wananchi na mali zao nchini upo vizuri.

Akizungumza katika kikao cha mabalozi hao waliofika ofisini kwake kwa nyakati tofauti leo, Lugola pia aliwaomba wawakilishi hao wa nchi zao hapa nchini waendelee kushirikiana na Wizara yake na nchi kwa ujumla.

Lugola aliwahakikishia Mabalozi hao kuwa Tanzania itaendelea kuwa salama kwa kuwa Wizara yake imejipanga vizuri kuendelea kuwalinda raia na mali zao pamoja na wageni wote waishio nchini. “Mheshimiwa Balozi nashukuru sana kwa kunitembelea, najisikia furaha kwa ujio wako na karibu sana wakati wowote, Wizara yangu pamoja na nchi yangu kwa ujumla tutaendelea kushirikiana nanyi katika masuala mbalimbali,” alisema Lugola.

Hata hivyo, Balozi wa Afrika Kusini, Thami Mseleku alisema akiwa nchini anajiona kuwa yupo nyumbani kwasababu nchi yake ina historia kubwa ya ushirikiano na Tanzania. Hata hivyo, Balozi wa Italia, Roberto Mengoni alimpongeza Waziri Lugola kwa kuteuliwa na Rais John Magufuli kuiongoza Wizara hiyo na pia alimuakikishia ushirikiano zaidi kati ya nchi yake na Tanzania.

“Hongera sana mheshimiwa Waziri kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani na pia nimefurahi kuja katika ofisini yako kufanya mazungumzo nawe,” alisema Balozi Mengoni. Naye Balozi wa Kenya Nchini, Dan Kazungu alisema Tanzania ni nchi yake na anajisikia furaha kuwepo nchini kwasababu alishawahi kufanyakazi miaka kadhaa iliyopita hapa nchini, hivyo nchi yake itaendelea kutoa ushirikiano katika masuala mbalimbali Tanzania.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akimfafanulia jambo Balozi wa Italia, Roberto Mengeni, kuhusiana na masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya nchi yake na Tanzania. Lugola alimuhakikishia Balozi huyo kuwa, Tanzania itaendelea kuwa salama na kuimarisha ushirikiano na Italia. Mazungumzo hayo yalifanyika ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam leo. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akimfafanulia jambo Balozi wa Afrika Kusini, Thami Mseleku, kuhusiana na masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya nchi yake na Tanzania. Lugola alimuhakikishia Balozi huyo kuwa, Tanzania itaendelea kuwa salama na kuimarisha ushirikiano na Afrika Kusini. Mazungumzo hayo yalifanyika ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam leo 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akimfafanulia jambo Balozi wa Italia, nje ya jengo la ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam, kabla ya kuagana na Balozi huyo baada ya kumaliza mazungumzo yao kuhusu masuala mbalimbali ya usalama wa nchi pamoja na ushirikiano kati ya Italia na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika jijini humo leo 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akimfafanulia jambo Balozi wa Kenya, Dan Kazungu kuhusiana na masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya nchi yake na Tanzania. Lugola alimuhakikishia Balozi huyo kuwa, Tanzania itaendelea kuwa salama na kuimarisha ushirikiano na Kenya. Mazungumzo hayo yalifanyika ofisi ndogo ya Wizara, jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 


Hivyo makala WAZIRI LUGOLA AWAAMBIA MABALOZI NCHI IPO SALAMA, AAHIDI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NAO

yaani makala yote WAZIRI LUGOLA AWAAMBIA MABALOZI NCHI IPO SALAMA, AAHIDI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NAO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI LUGOLA AWAAMBIA MABALOZI NCHI IPO SALAMA, AAHIDI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NAO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/waziri-lugola-awaambia-mabalozi-nchi.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "WAZIRI LUGOLA AWAAMBIA MABALOZI NCHI IPO SALAMA, AAHIDI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NAO"

Post a Comment

Loading...