Loading...

WAZIRI LUKUVI APIGA MARUFUKU HALMASHAURI NCHINI KUSHINIKIZWA KUPIMA VIWANJA NA WAMILIKI MASHAMBA

Loading...
WAZIRI LUKUVI APIGA MARUFUKU HALMASHAURI NCHINI KUSHINIKIZWA KUPIMA VIWANJA NA WAMILIKI MASHAMBA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI LUKUVI APIGA MARUFUKU HALMASHAURI NCHINI KUSHINIKIZWA KUPIMA VIWANJA NA WAMILIKI MASHAMBA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI LUKUVI APIGA MARUFUKU HALMASHAURI NCHINI KUSHINIKIZWA KUPIMA VIWANJA NA WAMILIKI MASHAMBA
link : WAZIRI LUKUVI APIGA MARUFUKU HALMASHAURI NCHINI KUSHINIKIZWA KUPIMA VIWANJA NA WAMILIKI MASHAMBA

soma pia


WAZIRI LUKUVI APIGA MARUFUKU HALMASHAURI NCHINI KUSHINIKIZWA KUPIMA VIWANJA NA WAMILIKI MASHAMBA

Na Munir Shemweta, Babati
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amepiga marufuku halmashauri zote nchini kupima viwanja kwa shinikizo la wamiliki wa mashamba makubwa na kusisitiza kuwa kazi hiyo inapaswa kufanywa na  halmashauri ambazo ndizo zenye jukumu la kupanga miji nchini.

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Singu wilaya ya Babati mkoani Manyara Lukuvi alisema uamuzi wowote wa kupima viwanja unatakiwa kuratibiwa na halmashauri husika kwa kuzingatia mipango miji na si vinginevyo kwa kuwa mwenye  dhamana ya kupanga miji ni halmashauri. Agizo la Waziri Lukuvi linafuatia kuelezwa na halmashauri za wilaya ya Babati kuhusu mpango wa kupima viwanja katika eneo la shamba la Singu Estate linalomilikiwa na kampuni ya Agric Evolution Ltd .

Lukuvi ameziagiza halmshauri za Mji na ile ya wilaya ya Babati kuainisha mipaka na kupima eneo la vijiji vya Singu, Sigino na Daglailoy vilivyopo kata ya Singu wilaya ya Babati sambamba na kuvipatia hati vijiji vyote na kubainisha kuwa zoezi la kugawa viwanja katika  shamba linalomilikiwa na kampuni ya Agric Evolution ltd litafanyika baadaye kwa utaratibu utakaopangwa.

Lukuvi alisema ameamua kusitisha ugawaji viwanja baada ya kubaini ukiukwaji wa taratibu sambamba na baadhi ya wawekezaji kununua mashamba katika maeneo ya mjini kwa nia ya kuzishawishi halmshauri kupima viwanja badala ya halmashauri kupima kulingana na mipango yake. " kumekuwa na mtindo wamiliki wa mashamba wanachukua maeneo ambayo wanaona yanakaribia kuwa miji kwa lengo la kupima viwanja na kuwalambisha asali  watendaji wa halmashauri ili malengo yao yatimie" alisema Lukuvi.
 Waziri wa Ardhi Nyumba na Mendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza na wananchi wa kijiji cha Singu wilaya ya Babati mkoani Manyara wakati wa ziara ya siku moja kutatua mgogoro  wa ardhi baina ya wananchi na wamiliki wa mashamba ya Singu na Endasago.
 Mbunge wa jimbo la Babati Paulina Gekul akitoa shukuran kwa  Waziri wa Ardhi Nyumba na Mendeleo ya Makazi William Lukuvi kwa kutatua mgogoro wa ardhi uliodumu kwa zaidi ya miaka 30 baina ya wananchi wa Singu na Endasago na wamiliki wa mashamba ya Singu na Endasago.

 Wananchi wa vijiji vya Endasago na Dudiye vilivyopo wilaya ya Babati mkoa wa Manyara wakimsikiliza Waziri wa Ardhi Nyumba na Mendeleo ya Makazi William Lukuvi wakati wa ziara ya siku moja kutatua mgogoro wa ardhi baina ya wananchi na wamiliki wa mashamba ya Singu na Endasago.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Mendeleo ya Makazi William Lukuvi akifurahia jambo na mbunge wa jimbo la Babati Paulina Gekul (kulia) wakati wa ziara ya siku moja kutatua mgogoro wa ardhi  baina ya wananchi na wamiliki wa mashamba ya Singu na Endasago. Co Ltd.(Picha zote na Wizara ya Ardhi)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala WAZIRI LUKUVI APIGA MARUFUKU HALMASHAURI NCHINI KUSHINIKIZWA KUPIMA VIWANJA NA WAMILIKI MASHAMBA

yaani makala yote WAZIRI LUKUVI APIGA MARUFUKU HALMASHAURI NCHINI KUSHINIKIZWA KUPIMA VIWANJA NA WAMILIKI MASHAMBA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI LUKUVI APIGA MARUFUKU HALMASHAURI NCHINI KUSHINIKIZWA KUPIMA VIWANJA NA WAMILIKI MASHAMBA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/waziri-lukuvi-apiga-marufuku_23.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "WAZIRI LUKUVI APIGA MARUFUKU HALMASHAURI NCHINI KUSHINIKIZWA KUPIMA VIWANJA NA WAMILIKI MASHAMBA"

Post a Comment

Loading...