Loading...

BALOZI SEIF AFANYA MAZUNGUMZO NA UONGOZI WA CHUO CHA KIMATAIFA CHA SAYANSI NA BIASHARA CHA NCHINI OMAN

Loading...
BALOZI SEIF AFANYA MAZUNGUMZO NA UONGOZI WA CHUO CHA KIMATAIFA CHA SAYANSI NA BIASHARA CHA NCHINI OMAN - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa BALOZI SEIF AFANYA MAZUNGUMZO NA UONGOZI WA CHUO CHA KIMATAIFA CHA SAYANSI NA BIASHARA CHA NCHINI OMAN, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : BALOZI SEIF AFANYA MAZUNGUMZO NA UONGOZI WA CHUO CHA KIMATAIFA CHA SAYANSI NA BIASHARA CHA NCHINI OMAN
link : BALOZI SEIF AFANYA MAZUNGUMZO NA UONGOZI WA CHUO CHA KIMATAIFA CHA SAYANSI NA BIASHARA CHA NCHINI OMAN

soma pia


BALOZI SEIF AFANYA MAZUNGUMZO NA UONGOZI WA CHUO CHA KIMATAIFA CHA SAYANSI NA BIASHARA CHA NCHINI OMAN

Uongozi wa Chuo cha Kimataifa cha Sayansi na Biashara cha Nchini Oman umekusudia kuanzisha chuo chengine kipya cha Kimataifa Visiwani Zanzibar kitachopewa jina la American and Europe of  East Africa kwa lengo la kutanua Sekta ya Elimu ndani ya Ukanda wa Afrika Mashariki.

Mkuu wa Chuo cha Sayansi na Biashara cha Nchini humo Dr. Muneer Moh’d Al – Naamany alitoa kauli hiyo wakati Ujumbe aliouongoza wa Chuo hicho ulipofanya mazungumzo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Vuga Mjini Zanzibar.

Dr. Muneer Moh’d Al – Mastar alisema Zanzibar lazima iwe kituo cha Elimu katika Ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Bara la Afrika kitakachomjengea uwezo wa ajira ya kuaminika mahali popote Duniani Mwanafunzi aatakayemaliza masomo yake kwenye Chuo hicho.

Alisema mazingira ya kumfinyanga Mwanafunzi katika muelekeo wa chuo hicho kinachokusudiwa kuanzishwa Zanzibar unatokana na uzoefu wa miaka 20 tokea kuanzishwa kwa Chuo chao chenye Wahadhiri kutoka pembe zote za Dunia wanaofundisha kwenye Taasisi yao.

Mkuu huyo wa Chuo cha Sayansi na Biashara cha Oman mwenye Asili ya Zanzibar alimueleza Balozi Seif kwamba Uongozi wa Chuo chake umefikiria Mpango huo kwa nia ya kuirejeshea hadhi yake Zanzibar kuwa Kituo cha masuala mengi katika enzi zilizopita hasa harakati za Biashara na usafiri uliokuwa ukiunganisha Dunia.

Naye kwa upande wake Naibu Mkuu wa Chuo cha Sayansi na Biashara cha Nchini Oman Dr. Ahmed Al – Naamany alisema mfumo wa ufundishaji utakaotumika utampa uwezo Mwanafunzi kuendelea na masomo yake hata akiwa nje ya Zanzibar.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Kulia akizungumza na Uongozi wa Chuo cha Kimataifa cha Sayansi na Biashara  cha Nchini Oman uliofika Ofisini kwake Vuga kwa mazungumzo ya kuataka kuanzisha Chuo Kikuu Visiwani Zanzibar.
 Mkuu wa Chuo cha Sayansi na Biashara cha Nchini humo Dr. Muneer Moh’d Al – Naamany wa Pili kutoka Kulia akielezea msimamo wa Uongozi wa Chuo chake kutaka kuanzisha Chuo Kikuu Visiwani Zanzibar.
 Dr. Muneer Moh’d Al – Naamany akisisitiza jambo wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Vuga Mjini Zanzibar.
 Naibu Mkuu wa Chuo cha Sayansi na Biashara cha Nchini Oman Dr. Ahmed Al – Naamany akimueleza Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh. Riziki Pembe Juma aliyeshiriki mazungumzo hayo fursa zitakazopatikana katika mafunzo yatakayotolewa na Chuo hicho.
  Dkt. Muneer Moh’d Al – Naamany akifafanua zaidi malengo ya Chuo chake mbele ya  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Vuga Mjini Zanzibar.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala BALOZI SEIF AFANYA MAZUNGUMZO NA UONGOZI WA CHUO CHA KIMATAIFA CHA SAYANSI NA BIASHARA CHA NCHINI OMAN

yaani makala yote BALOZI SEIF AFANYA MAZUNGUMZO NA UONGOZI WA CHUO CHA KIMATAIFA CHA SAYANSI NA BIASHARA CHA NCHINI OMAN Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala BALOZI SEIF AFANYA MAZUNGUMZO NA UONGOZI WA CHUO CHA KIMATAIFA CHA SAYANSI NA BIASHARA CHA NCHINI OMAN mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/balozi-seif-afanya-mazungumzo-na.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "BALOZI SEIF AFANYA MAZUNGUMZO NA UONGOZI WA CHUO CHA KIMATAIFA CHA SAYANSI NA BIASHARA CHA NCHINI OMAN"

Post a Comment

Loading...