Loading...

WAZIRI LUKUVI 'AWATUMBUA' MAAFISA ARDHI WATATU JIJI LA ARUSHA

Loading...
WAZIRI LUKUVI 'AWATUMBUA' MAAFISA ARDHI WATATU JIJI LA ARUSHA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI LUKUVI 'AWATUMBUA' MAAFISA ARDHI WATATU JIJI LA ARUSHA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI LUKUVI 'AWATUMBUA' MAAFISA ARDHI WATATU JIJI LA ARUSHA
link : WAZIRI LUKUVI 'AWATUMBUA' MAAFISA ARDHI WATATU JIJI LA ARUSHA

soma pia


WAZIRI LUKUVI 'AWATUMBUA' MAAFISA ARDHI WATATU JIJI LA ARUSHA

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amewasimamisha kazi watumishi watatu wa sekta ya ardhi katika halmashauri ya Jiji la Arusha kwa tuhuma ya kushirikiana na matapeli wa viwanja katika jiji hilo.

Aidha, Lukuvi ameagiza maofisa hao waliosimamishwa kazi kutokanyaga katika eneo la ofisi za Jiji mpaka hapo uchunguzi utakapofanyika na maamuzi dhidi ya tuhuma zao yatakapotolewa.

Lukuvi alichukua uamuzi huo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika ofisi za Jiji la Arusha jana kufuatia kuwepo tuhuma nyingi za matapeli ya viwanja kushirikiana na baadhi ya maofisa wa ardhi wasiokuwa waaminifu kufanya utapeli kwa wamiliki halali wa viwanja.Maafisa ardhi waliosimamishwa kwa tuhuma hizo za kushirikiana na matapeli kudhulumu viwanja kwa wamiliki halali katika jiji la Arusha ni Elizabeth Mollel, Lassen Mjema na Zawadi Mtafikikolo.

Mbali na kusimamishwa kazi kwa watumishi, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliagiza maafisa Ardhi wa Jiji la Arusha kuhakikisha matapeli wote wa viwanja wanaoshirikiana na watumishi hao wasipatiwe huduma katika masuala yoyote ya ardhi kufuatia kuonekana kujihusisha na mipango ya utapeli wa viwanja kwa kushirikiana na baadhi ya watumishi wa sekta ya ardhi katika jiji la Arusha.

Katika ziara yake hiyo ya kushtukiza pamoja na kuelezwa na Afisa Ardhi Mteule wa Jiji la Arusha Dicley Nyato uwepo wa watumishi wawili Lassen na Zawadi huku Elizabeth akiwa katika likizo ya uzazi, watumishi hao walipotea ghafla ofisini bila taarifa mara baada ya kuelezwa wanahitajika kwa waziri na hata pale walipopigiwa simu za mkononi hazikupatikana.

Kwa mujibu wa Lukuvi, watumishi hao wa sekta ya ardhi katika jiji la Arusha wamekuwa na mawasiliano ya mara kwa mara na matapeli wa viwanja katika jiji hilo jambo linalotia mashaka utendaji wao wa kazi na kubainisha kuwa maafisa hao wamekuwa na tabia ya kufuatilia kesi zilizopo katika Mabaraza ya Ardhi kwa nia ya kuwasaidia matapeli.



Hivyo makala WAZIRI LUKUVI 'AWATUMBUA' MAAFISA ARDHI WATATU JIJI LA ARUSHA

yaani makala yote WAZIRI LUKUVI 'AWATUMBUA' MAAFISA ARDHI WATATU JIJI LA ARUSHA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI LUKUVI 'AWATUMBUA' MAAFISA ARDHI WATATU JIJI LA ARUSHA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/waziri-lukuvi-awatumbua-maafisa-ardhi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WAZIRI LUKUVI 'AWATUMBUA' MAAFISA ARDHI WATATU JIJI LA ARUSHA"

Post a Comment

Loading...