Loading...
title : WAZIRI UMMY AAGIZA HOSPITALI ZOTE ZA RUFAA ZA MIKOA KUTOA MATIBABU YA KINYWA NA MENO.
link : WAZIRI UMMY AAGIZA HOSPITALI ZOTE ZA RUFAA ZA MIKOA KUTOA MATIBABU YA KINYWA NA MENO.
WAZIRI UMMY AAGIZA HOSPITALI ZOTE ZA RUFAA ZA MIKOA KUTOA MATIBABU YA KINYWA NA MENO.
Na WAMJW - MARA.
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amemwagiza Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya kuhakikisha kuwa kabla ya March 30, 2019 Hospitali zote za Mikoa kutoa Huduma za matibabu ya kinywa.
Ameyasema hayo wakati akifungua Mkutano wa Mwaka wa Madaktari wa Kinywa wenye lengo la kujadili njia bora za kuboresha huduma za Afya ya kinywa na meno na namna ya kuikuza kada hiyo, tukio lililofanyika katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Mara.
Waziri Ummy alisema kuwa "hatuwezi kusema kuwa Afya ya kinywa na meno ni muhimu alafu leo ni Hospitali za rufaa za Mikoa 10 kati ya 28 ndio zinavitendea kazi" alisema Waziri Ummy.Pia Waziri Ummy aliwahasa Wananchi kupambana dhidi ya magonjwa ya kinywa na meno kwa kujiepusha matumizi ya sigara, tumbaku, unywaji wa pombe kupita kiasi, ulaji wa vyakula na vinywaji vyenye sukari.
"Magonjwa ya kinywa na meno yana visababishi vyake ikiwemo uvutaji wa sigara,sigara, tumbaku, unywaji wa pombe kupita kiasi, ulaji wa vyakula na vinywaji vyenye Sukari" alisema Waziri Ummy.Kwa upande mwingine Mhe. Ummy amewataka madaktari wa kinywa na meno kuwahamasisha wananchi ili kufahamu umuhimu wa kupiga mswaki japo mara mbili kwa siku ili kujiepusha katika hatari yakupata magonjwa ya kinywa na meno.
"Mnatuambia kwamba angalau tupige mswaki mara mbili kwa siku, hapo mnakazi kubwa sana ya kutushawishi, hivyo niwaombe tushirikiane nasi ili kuhakikisha kwamba tunaongeza elimu na hamasa kwa jamii katika suala hiki" alisema Waziri Ummy.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akiambatana na kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Mara, wakiendelea na ukaguzi wa jengo la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa inayoendelea kujengwa.
Muonekano wa Jengo la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara inayoendelea kujengwa, ikiwa ni jitihada za Serikali ya awamu ya tano kuboresha Sekta ya Afya nchini.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu (aliyesimama katikati) akiteta jambo na kamati kuu ya usalama ya Mkoa iliyoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe.Adam Malima wakati wa ukaguzi wa jengo la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara inayoendelea kujengwa.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee hma Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akisisitiza jambo mbele ya Madaktari wa Afya ya kinywa na meno (hawapo kwenye picha) wakati akifungua mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Mara.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

Hivyo makala WAZIRI UMMY AAGIZA HOSPITALI ZOTE ZA RUFAA ZA MIKOA KUTOA MATIBABU YA KINYWA NA MENO.
yaani makala yote WAZIRI UMMY AAGIZA HOSPITALI ZOTE ZA RUFAA ZA MIKOA KUTOA MATIBABU YA KINYWA NA MENO. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI UMMY AAGIZA HOSPITALI ZOTE ZA RUFAA ZA MIKOA KUTOA MATIBABU YA KINYWA NA MENO. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/waziri-ummy-aagiza-hospitali-zote-za.html
0 Response to "WAZIRI UMMY AAGIZA HOSPITALI ZOTE ZA RUFAA ZA MIKOA KUTOA MATIBABU YA KINYWA NA MENO."
Post a Comment