Loading...
title : BATA WAPEWE THAMANI KAMA JAMII ZINGINE ZA NDEGE ILI KULETA UFUGAJI WENYE TIJA
link : BATA WAPEWE THAMANI KAMA JAMII ZINGINE ZA NDEGE ILI KULETA UFUGAJI WENYE TIJA
BATA WAPEWE THAMANI KAMA JAMII ZINGINE ZA NDEGE ILI KULETA UFUGAJI WENYE TIJA
Na Khadija Seif, Globu ya Jamii
UMOJA wa wafugaji bata nchini wamekutana na kuzindua tamasha la uchomaji wa nyama ya Bata katika ukumbi wa police officers mess jijini Dar es salaam.
Akifungua hafla hiyo ya tamasha la uchomaji nyama ya bata Afisa mifugo wa jamii ya ndege Deodratus Nestory kutoka Manispaa ya Kinondoni
amewapongeza wafugaji hao na kusema kuwa ni nadra sana kukuta tamasha la uchomaji nyama ya bata kwani imeshazoeleka mbuzi choma na kuku choma.
Nestory amesema kuwa "Umoja huu upo kwa ajili ya kutia watu hamasa ili waweze kutambua thamani ya nyama ya bata, na Manispaa ya Kinondoni itatoa semina kwa wafugaji wote wa mbuzi,ngombe, kuku na bata ili waweze kupata masoko kwa urahisi na kuwapa ushirikiano kutoka Serikalini kuanzia Manispaa hadi Wizara husika ya Kilimo na ufugaji" amesema Nestory.
Pia Nestory amefafanua kuwa kufikia mwakani watafungua chama cha wafugaji wa jamii ya ndege ambacho kitatambulika kisheria
Ili waweze kupata mkopo kutoka mabenki tofauti na kuwawezesha kupanua soko na ufugaji wenye tija.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo iliyowakutanisha wafugaji wa Bata kutoka sehemu mbalimbali yakiwemo Kawe, Kibiti,Morogoro,kigamboni na Bunju Mwenyekiti wa chama hicho Riziki osward amesema sasa ni wakati wa kumpa thamani bata pamoja na nyama ya bata kwani jamii bado haina mwamko katika Kula kwa wingi nyama hiyo.
Hata hivyo osward amefafanua zaidi kuwa lengo la tamasha hilo sio tu Kula nyama peke yake bali hata kujifunza namna bora ya kufuga bata hao hasa katika kuanzia malisho ,madawa na chakula.
Pia ameeleza kuwa mikakati ya Umoja wa wafugaji bata itahakikisha inatoa elimu kwa wafugaji na kuwasaidia ili kuweza kupanua soko na kumpa thamani bata kwani bado kuna desturi iliyojengeka juu ya bata kuwa ni mchafu japo bata ana thamani kubwa kuliko kuku .
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala BATA WAPEWE THAMANI KAMA JAMII ZINGINE ZA NDEGE ILI KULETA UFUGAJI WENYE TIJA
yaani makala yote BATA WAPEWE THAMANI KAMA JAMII ZINGINE ZA NDEGE ILI KULETA UFUGAJI WENYE TIJA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BATA WAPEWE THAMANI KAMA JAMII ZINGINE ZA NDEGE ILI KULETA UFUGAJI WENYE TIJA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/bata-wapewe-thamani-kama-jamii-zingine.html
0 Response to "BATA WAPEWE THAMANI KAMA JAMII ZINGINE ZA NDEGE ILI KULETA UFUGAJI WENYE TIJA"
Post a Comment