Loading...
title : NMB YAITOA MABATI 229 KUPIGA TAFU UJENZI WODI YA WAKINA MAMA HOSPITALI YA WILAYA YA MUHEZA
link : NMB YAITOA MABATI 229 KUPIGA TAFU UJENZI WODI YA WAKINA MAMA HOSPITALI YA WILAYA YA MUHEZA
NMB YAITOA MABATI 229 KUPIGA TAFU UJENZI WODI YA WAKINA MAMA HOSPITALI YA WILAYA YA MUHEZA
BENKI ya NMB nchini imetoa mabati 229 kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya wakima mama katika hospitali ya wilaya ya Muheza ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt John Magufuli kuhakikisha wananchi wanaondokana na changamoto za afya kwenye maeneo yao.
Hafla ya makabidhiano hayo yalifanyika mjini Muheza na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa maendeleo akiwemo Katibu wa UWT Mkoani Tanga Sophia Nkupe na Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo.
Akizungumza baada ya kupokea mabati hayo Katibu wa UWT huyo aliishukuru na kuwapongeza benki ya NMB kwa kuwakubalia ombi lao la kuwasaidia mabati kwa sababu wamekuiwa mstari wa mbele kusaidia lakini wanafanya hivyo kuunga mkono juhudui za Rais katika dhamirta yake ya kuhakikisha huduma za afya zinakuwa bora,.
Nkupe alisema pia wana mpongeza Rais Dkt John Magufuli kwa juhudi kubwa anazofanya kuhakikisha wananchi wanaondokana na changamoto mbalimbali ikiwemo za huduma ya afya na nyenginevyo
“Lakini pia nikushukuru Mh DC Mhandisi Mwanasha Tumbo kwa juhudi zako unazozifanya kuhakikisha wilaya ya Muheza inapata maendeleo makubwa pia niwaombe NMB mtusaidie wakina mama kwa sababu tunateseka sana wanachombezwa na taasisi mbalimbali za mikopo yenye riba kubwa”Alisema Katibu huyo wa UWT.
Kaimu Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini Cosmas Gabriel kushoto akimkabidhi mabati 229 Katibu wa UWT Mkoani Tanga Sophia Nkupe kwa ajili ya ujenzi wa wodi wakina mama hospitali ya wilaya ya Muheza kulia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo
Katibu wa UWT Mkoani Tanga Sophia Nkupe kulia akimkabidhi 229 Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo mabati 229 kwa ajili ya ujenzi wa wodi wakina mama hospitali ya wilaya ya Muheza kushoto ni Kaimu Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini Cosmas Gabriel
Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo kushoto akimkabidhi mabati 229 Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza kwa ajili ya ujenzi wa wodi wakina mama hospitali ya wilaya ya Muheza kushoto ni Kaimu Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini Cosmas Gabriel
Katibu wa UWT Mkoani Tanga Sophia Nkupe akizungumza katika halfa hiyo kulia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo
Hivyo makala NMB YAITOA MABATI 229 KUPIGA TAFU UJENZI WODI YA WAKINA MAMA HOSPITALI YA WILAYA YA MUHEZA
yaani makala yote NMB YAITOA MABATI 229 KUPIGA TAFU UJENZI WODI YA WAKINA MAMA HOSPITALI YA WILAYA YA MUHEZA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NMB YAITOA MABATI 229 KUPIGA TAFU UJENZI WODI YA WAKINA MAMA HOSPITALI YA WILAYA YA MUHEZA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/nmb-yaitoa-mabati-229-kupiga-tafu.html
0 Response to "NMB YAITOA MABATI 229 KUPIGA TAFU UJENZI WODI YA WAKINA MAMA HOSPITALI YA WILAYA YA MUHEZA"
Post a Comment