Loading...
title : BITEKO AICHARUKIA KAMPUNI YA UCHIMBAJI MADINI KIJIJI CHA MANGAE , WILAYANI MVOMERO
link : BITEKO AICHARUKIA KAMPUNI YA UCHIMBAJI MADINI KIJIJI CHA MANGAE , WILAYANI MVOMERO
BITEKO AICHARUKIA KAMPUNI YA UCHIMBAJI MADINI KIJIJI CHA MANGAE , WILAYANI MVOMERO
Na Mwadishi wetu, Morogoro
NAIBU Waziri wa Madini, Doto Biteko ameiagiza Menajimenti ya Kampuni ya MMC ya uchimbaji wa dhahabu katika kijiji ch Mangae wilayani Mvomero, mkoani Morogoro kusimamisha uchimbaji hadi itakapokamilisha taratibu za kisheria za Serikali zinazosimamia madini pamoja na kuwalipa fidia wananchi waliohamishwa meneo yao waliokuwa wakiishi.
Biteko alitoa agizo hilo baada ya kufanya ziara ya kukagua shughuli zinazofanywa na Kampuni hiyo kwenye eneo la mgodi huo uliopo katika vijiji vya Mtupule na Mangae na kubaini imekuwa ikeindelea kuchimba madini ya dhahabu kinyume na sheria licha ya kutakiwa kukamilisha kwanza utaratibu waliopewa wa kisheria .
Mbali na hilo , Naibu Waziri alionya na kutoa wito kwa Watanzania wote wanapoamua kuingia mikataba na mikataba ya wachimbaji wadogo ni lazima itambuliwe na serikali kwa mujibu wa sheria ya uwekezaji sekta ya madini na si vinginevyo.
Naibu Waziri alisema , kufuatwa kwa sheria na utaratibu wa mikataba na wawekezaji wa n je inalenga kuwalinda uwekezaji wao ili baadaye wasione wananyanyaswa pale mikataba walioingia na watu wasio waaminifu inakinzana na sheria mpya ya madini
Hata hivyo alisema , manufaa ya madini kwa wananchi wa eneo hilo hayawezi kupatikana endapo mahusiano kati ya mgodi na wananchi hayatakuwa mazuri na kwamba rasilimali za nchi lazima ziwanufaishe Watanzania wote yakiwemo Madini.
Mkazi wa kijiji cha Mangae , kata ya Mangae, wilayani Mvomero mkoani Morogoro, Anita John akitoa malalamiko yake kwa Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ( hayupo pichani ) kuhusu Kampuni ya MMC ya uchimbaji wa dhahabu katika eneo la kijiji hicho kuendesha shughili zao pasipo kuwafidia makazi yao waliyokuwa wakiishi kupisha uchimbaji wake.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko akisoma baadhi ya nyaraka za Kampuni ya MMC ya uchimbaji wa dhahabu katika kijiji cha Mangae wilayani Mvomero, mkoani Morogoro wakati wa ziara ya kukagua shughuli zinazofanywa na Kampuni hiyo na ( wapili kulia) ni Mkuu wa wilaya hiyo, Mohamed Utaly.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ( aliyeweka mikono mfukoni) akipewa maelezo na kuangalia mashine za Kampuni ya MMC zilizofungwa kwenye mgodi wa uchimbaji wa dhahabu katika kijiji cha Mangae wilayani Mvomero, mkoani Morogoro wakati wa ziara ya kukagua shughuli zinazofanywa na Kampuni hiyo.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ( aliyeweka mikono mfukoni) akiteremka chini kutoka kuangalia mashine za Kampuni ya MMC zilizofungwa kwenye mgodi wa uchimbaji wa dhahabu katika kijiji cha Mangae wilayani Mvomero, mkoani Morogoro wakati wa ziara ya kukagua shughuli zinazofanywa na Kampuni hiyo.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala BITEKO AICHARUKIA KAMPUNI YA UCHIMBAJI MADINI KIJIJI CHA MANGAE , WILAYANI MVOMERO
yaani makala yote BITEKO AICHARUKIA KAMPUNI YA UCHIMBAJI MADINI KIJIJI CHA MANGAE , WILAYANI MVOMERO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BITEKO AICHARUKIA KAMPUNI YA UCHIMBAJI MADINI KIJIJI CHA MANGAE , WILAYANI MVOMERO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/biteko-aicharukia-kampuni-ya-uchimbaji.html
0 Response to "BITEKO AICHARUKIA KAMPUNI YA UCHIMBAJI MADINI KIJIJI CHA MANGAE , WILAYANI MVOMERO"
Post a Comment