Loading...
title : BODI YA MAJI YAFYEKA MAZAO YA WAKULIMA MTO RUVU
link : BODI YA MAJI YAFYEKA MAZAO YA WAKULIMA MTO RUVU
BODI YA MAJI YAFYEKA MAZAO YA WAKULIMA MTO RUVU
Bodi ya Maji Bonde la Wami/ Ruvu imefika na kufyeka mazao mbalimbali yaliyolimwa pembezoni mwa Mto Ruvu na ndani ya Mita 60 kutoka kwenye mto huo katika eneo la Ruvu Darajaji mkoani Pwani.
Akizungumza na waandishi wa habari, Afisa Maji wa Bonde la Wami/Ruvu, Simon Ngonyani amesema kuwa zoezi hilo ni muendelezo wa operation ya kuwaondoa watu wanaofanya shughuli za kibinadamu ikiwemo kilimo na kujenga makazi yao ndani ya Mita 60 kutoka Mto huo ili kulinda chanzo hicho cha maji.
"Sasahivi maji yamepungua katika Mto huu nilikuwa naongea na ndugu yangu CEO wa DAWASA aliniambia kwamba mitambo yake sasa inaungua kwasababu kina cha maji kimepungua sana na maji yanapungua kwasababu watu wanalima hivyo michanga inaingia kwenye mto kina kinapingua" -Ngonyani.
Aidha amesema kuwa kutokana na wakulima hao wanaolima kando ya Mto kwa kutumia mbolea za chumvi chumvi kunapelekea usalama wa maji hayo kupotea kwa watumiaji hivyo watu wafuate sheria ili kulinda maji ya Mto huo.
"Tumeamua kusimamia sheria hatutawabakisha, leo tunafyeka mazao yote yaliyopo ndani ya Mita 60 lakini kinachofuatia nyumba ambazo zipo ndani ya Mita 60 zenyewe pia tutazifanyia kazi"- Ngonyani.
Afisa Maji Bodi ya Maji Bonde la wami/Ruvu Simon Ngonyani (wa kwanza kulia) akiongoza zowezi la kufyeka mazoo mbalimbali yaliyolimwa ndani ya mita 60 pembezoni mwa mto Ruvu leo mkoa wa Pwani..(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)
Muonekano wa mazoo yaliyolimwa ndani ya mita 60 pembezoni mwa mto Ruvu mkoa wa Pwani.
Ufyekaji wa mazao yaliyolimwa ndani ya mita 60 pembezoni mwa mto Ruvu mkoa wa pwani ukiendelea.
Muonekano wa mto Ruvu uliopo mkoa wa Pwani.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)
Hivyo makala BODI YA MAJI YAFYEKA MAZAO YA WAKULIMA MTO RUVU
yaani makala yote BODI YA MAJI YAFYEKA MAZAO YA WAKULIMA MTO RUVU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BODI YA MAJI YAFYEKA MAZAO YA WAKULIMA MTO RUVU mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/bodi-ya-maji-yafyeka-mazao-ya-wakulima.html
0 Response to "BODI YA MAJI YAFYEKA MAZAO YA WAKULIMA MTO RUVU"
Post a Comment