Loading...

TRA YANG'ARA TUZO YA NBAA, WAPATA USHINDI WA JUMLA.

Loading...
TRA YANG'ARA TUZO YA NBAA, WAPATA USHINDI WA JUMLA. - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TRA YANG'ARA TUZO YA NBAA, WAPATA USHINDI WA JUMLA., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TRA YANG'ARA TUZO YA NBAA, WAPATA USHINDI WA JUMLA.
link : TRA YANG'ARA TUZO YA NBAA, WAPATA USHINDI WA JUMLA.

soma pia


TRA YANG'ARA TUZO YA NBAA, WAPATA USHINDI WA JUMLA.



Mkurugenzi wa Fedha Mamlaka wa Mapato Tanzania (TRA) Dinah Edward (kushoto) akipewa tuzo kutoka kwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Ashatu Kijaji baada ya kutangazwa na Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) wamekuwa washindi katika kutengeneza vitabu bora katika Mamlaka ya Serikali.
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imefanikiwa kushinda tuzo mbili ikiwemo mshindi wa jumla kutoka Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) ambazo wametolewa kwa taasisi, kampuni pamoja na mashirika mbalimbali ambayo yamefanya vizuri katika kuandaa taarifa za fedha katika utendaji wao.

Tuzo hizo walizopata TRA ni kuandaa vitabu  bora za fedha katika Mamlaka za Serikali pamoja na kuwa mshindi wa jumla katika kutengeneza vitabu bora vya fedha kwa kufata viwango na utaratibu wa kimataifa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam baada NBAA kuwatangaza TRA kuwa washindi wa jumla katika mashinda hayo Kamshna wa TRA Charles Kichele, amesema kuwa ushindi huo umetokana na kutengeneza vitabu vyao kwa kufata utaratibu na viwango vya kimataifa vinavyotumika kutengeneza hasebu za serikali.

Kichele amesema kuwa vitabu vyao vimeonekana vizuri kuliko vitabu vingine vilivyotengenezwa kutoka taasisi nyengine zote.

"Siri ya mafanikio yetu ni ushirikiano na kujituma katika utendaji wa wetu wa kazi, kuna wakati tunafanya kazi hadi muda wa ziada" amesema Kamishna Kichele.

Kamshna Kichele amefafanua kuwa wahasibu wa TRA wamekuwa wakitumia muda wa ziada ili kuhakikisha vitabu vinavyoandaliwa vinakuwa na ubora.

Ameeleza kuwa jitiada za wahasibu wa TRA zimeweza kuwapa ushindi wa jumla katika kuhakikisha wamefanya kazi yao katika viwango vinavyo stahili.

"Nawashukuru wahasibu TRA. pamoja na mkurugenzi wa fedha kwa kazi nzuri walizofanya" amesema Kamshna Kichele.

Katika hatua nyengine Kamshna Kichele amewata wafanyabiashara kuwa na utamaduni wa kuandaa vitabu  vyao vizuri jambo ambalo litasaidia kuandaa taarifa za fedha kwa ubora na kuleta maendeleo ya kiuchumi katika utendaji wao.

"Ni vizuri mamlaka, taasisi, makampuni wakajitaidi kuandaa taarifa za fedha kwa kutimiza viwango ili waweze kufika malengo ya TRA" amesema Kamishna Kichele.

Awali Mgeni rasmi katika hafla ya utoaji wa tuzo hizo, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Ashatu Kijaji, amesema kuwa uandaaji wa taarifa za fedha kwa kufata utaratibu ni jambo la muhimu kutokana uleta ufanisi katika uchumi.

Dk. Kijaji amesema kuwa kwa sasa ajenda kuu ni maendeleo ya kufikia uchumi wa kati hadi kufika mwaka 2025.

"Kwa sasa tunapanga na kuangalia maendeleo ili kuhakikisha tunakuwa na uchumi mzuri" amesema Dk. Kijaji.

Ugawaji wa tuzo za NBBA zinazotambulika kwa jina 'Best presented financial statements for the years 20I7 zimefanyika Desemba 8 mwaka huu jijini Dar es Salaam.


Hivyo makala TRA YANG'ARA TUZO YA NBAA, WAPATA USHINDI WA JUMLA.

yaani makala yote TRA YANG'ARA TUZO YA NBAA, WAPATA USHINDI WA JUMLA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TRA YANG'ARA TUZO YA NBAA, WAPATA USHINDI WA JUMLA. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/tra-yangara-tuzo-ya-nbaa-wapata-ushindi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "TRA YANG'ARA TUZO YA NBAA, WAPATA USHINDI WA JUMLA."

Post a Comment

Loading...