Loading...
title : Brela yapewa siku 14 kuufanya marekebisho mfumo wa kielektroniki
link : Brela yapewa siku 14 kuufanya marekebisho mfumo wa kielektroniki
Brela yapewa siku 14 kuufanya marekebisho mfumo wa kielektroniki
Hussein Ndubikile
Mwamba wa habari
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji George Kakunda ameipa siku 14 Brela kuufanyia ukaguzi mfumo wa kielektroniki ili kubaini chanzo cha kushindwa kufanya kazi ipasavyo na kuwaondolea adha wafanyabiashara.
Agizo hilo amelitoa leo jijini Dar es Salaam alipotembelea Makao ya Ofisi za Brela kujionea utendaji na kusikliza changamoto wanazokabiliana nazo watumishi.
Amesema kuwa kumekuwa malalamiko mengi yanayotolewa na waaafanyabiashara kuhusiana na utendaji wa kusuakusua kwa mfumo huo hali inayosababisha wafanyabiashara kusshindwa kujisajili kwa mfumo wa kimtandao.
“ Natoa siku 14 mkague mifumo yote ya kielektroniki kama mtambo haufanyi kazi waiteni waliofunga wauanagalie na muwaeleze changamoto zake,” amesema.
Amebanisha kuwa huenda waaliofunga mtambo wa mfumo hawana nia njema na Brela na kwamba juhudi za dhati zifanyike kubaini chanzo cha tatizo hilo.
Waziri Kakunda ameigiza Brela kuweka kitengo cha kupokea malalamiko ya wateja kwa kuweka namba zitakazosaidia utatuzi wa changamoto.
Pia ameiagiza kutoa elimu kwa wananchi kupitia Redio, runinga ili shughuli zake ziweke kuatambulika kwa wananchi.
Maagizo mengine aliyoyatoa ni Brela kuweka utaratibu wa kuwatembelea wafanyabiashara ili kutatua changamoto zao, kurekebisha taarifa zisizo sahihi zilizomo ndani ya tovuti ya Brela pamoja na kurekebisha hali ya biashara.
Katika hatua nyingine, Waziri Kakunda ameitaka Brela kuacha tabia ya kushirikiana na vishoka wanaotumia mgongo wao kufanya utapeli.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Brela, Emanuel Kazwezwe amesema mamlaka hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo uchache wa watumishi, uelewa mdogo wa Tehama kwa wateja pamoja na vibali vya ajiri kuchelewa.
Hivyo makala Brela yapewa siku 14 kuufanya marekebisho mfumo wa kielektroniki
yaani makala yote Brela yapewa siku 14 kuufanya marekebisho mfumo wa kielektroniki Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Brela yapewa siku 14 kuufanya marekebisho mfumo wa kielektroniki mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/brela-yapewa-siku-14-kuufanya.html
0 Response to "Brela yapewa siku 14 kuufanya marekebisho mfumo wa kielektroniki"
Post a Comment