Loading...
title : TBS Yatoa Elimu kwa Wananchi 22,322
link : TBS Yatoa Elimu kwa Wananchi 22,322
TBS Yatoa Elimu kwa Wananchi 22,322
Na Neema Mtemvu - TBS
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limemaliza Kampeni yake ya kutoa Elimu kwa umma katika Wilaya ya Nachingwea, Kilwa, Songea, Bukoba, Kahama,Tarime, Nyamagana, Korogwe, Kilombero na Kisarawe juu ya umuhimu wa kununua bidhaa zilizothibitishwa na shirika hilo.
Kampeni hiyo ya Elimu kwa umma imefanyika katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya Shule za Msingi na Sekondari, Masoko, Stendi, Minadani na maeneo mengine ya wazi ambapo wananchi walijitokeza kupata elimu na ufahamu wa masuala mbalimbali yahusuyo Ubora wa Bidhaa.
Kwa upande wake Afisa Masoko Mwandamizi, Gladness Kaseka amewakumbusha Wananchi wote kuwa vita ya bidhaa hafifu sio ya TBS pekee bali ni ya Taifa kwa ujumla.
"Kampeni hii imeweza kuwafikia wananchi 22,322 kati yao wajasiriamali 437,wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari 6,653 na wananchi 15,232," Alisema Kaseka.
Aliwasisitiza wananchi kuendelea kutoa taarifa kupitia mawasiliano waliyopewa pale wanapogundua uwepo wa bidhaa hafifu katika soko.
Vilevile Shirika lilipata fursa ya kutoa semina kwa wajasiriamali wanaojihusisha na bidhaa mbalimbali zikiwemo za nafaka, sabuni,mikate, maziwa,pilipili,siagi ya karanga, karanga,korosho,mvinyo,mafuta ya kula,asali,batiki,vikoi na unga lishe juu ya utaratibu wa kupata leseni ya kutumia alama ya ubora ya TBS bure.
Kampeni hiyo imemalizikia katika Wilaya za Korogwe, Kilombero na Kisarawe.
Afisa Uhusiano (TBS) Neema Mtemvu akizungumzia umuhimu wa kununua bidhaa zilizothibitishwa ubora wake na TBS na wanafunzi wa shule ya msingi Malunga wilayani Kahama.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Sirari wilayani Tarime wakisikiliza masuala ya ubora wa bidhaa
Wajasiriamali wilayani korogwe wakifuatiliwa utaratibu wa kupatiwa leseni ya kutumia alama ya ubora bure.
Wajasiriamali wilayani Kisarawe wakisikiliza kwa makini utaratibu wa kufuata ili kupata leseni ya kutumia alama ya ubora ya TBS bure.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kibaoni wilayani Kilombero,wakisikiliza kwa makini masuala yahusuyo ubora wa bidhaa
Afisa Udhibiti Ubora Mwandamizi(TBS) Amina Yasin akizungumza na wananchi wa soko kuu la Ifakara, wilayani Kilombero, juu ya umuhimu wa kununua bidhaa zilizothibitishwa ubora wake na TBS.
Hivyo makala TBS Yatoa Elimu kwa Wananchi 22,322
yaani makala yote TBS Yatoa Elimu kwa Wananchi 22,322 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TBS Yatoa Elimu kwa Wananchi 22,322 mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/04/tbs-yatoa-elimu-kwa-wananchi-22322.html
0 Response to "TBS Yatoa Elimu kwa Wananchi 22,322"
Post a Comment