Loading...
title : Dk Mengi afungua milango ya ushirikiano na wawekezaji wa Kichina
link : Dk Mengi afungua milango ya ushirikiano na wawekezaji wa Kichina
Dk Mengi afungua milango ya ushirikiano na wawekezaji wa Kichina
Na Mwandishi wetu
Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dr Reginald Mengi amewaalika wafanyabiashara kutoka China washirikiane naye kuwekeza nchini kwa ubia katika miradi mbalimbali, wakati huu ambapo Tanzania inapojizatiti kuwa ya viwanda.
Dr Mengi ametoa rai hiyo jijini Dar es salaam wakati wa chakula cha mchana alichowaandalia wawakilishi wa makampuni 17 kutoka China waliopo nchini kutafuta fursa za uwekezaji, walioambatana kwenye hafla hiyo na Balozi wa China nchini Mhe. Wang Ke.
Amesema Tanzania ni nchi iliyojaaliwa fursa nyingi za uwekezaji kutokana na utajiri wake wa raslimali na kusisitiza kuwa waliotayari kushirikiana naye katika miradi mbalimbali kama ya ujenzi wa bomba la gesi kutoka Tanzania hadi Uganda wajitokeze.
Akizungumza katika hafla hiyo Balozi wa China nchini Mhe. Wang Ke amesema ofisi yake itakuwa kiunganishi baina ya Wafanyabiashara wa China na Dr Mengi katika kufanikisha pendekezo la kuanzisha kwa ubia hapa nchini viwanda mbalimbali.
Kiongozi wa Ujumbe wa wafanyabiashara hao Bw. Lyu Xinhua amesema amekuja na ujumbe kutoka makampuni 17 ya China yanahusika na shughuli mbalimbali kuanzia ujenzi wa miundombinu, uhandisi, teknolojia ya mawasiliano nk, na kuahidi kuwasilisha mapendekezo yaliyotolewa kwa makampuni husika kwa ajili ya hatua zaidi za utekelezaji.
Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Dr. Reginald Mengi akizungumza wakati wa chakula cha mchana alichowaandalia wawakilishi wa makampuni 17 kutoka China waliopo nchini kutafuta fursa za uwekezaji katika hafla fupi iliyofanyika Serena Hotel jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Uanachama wa Tanzania Private Sector Foundation (TPSF), Bw. Louis Accaro, Kiongozi wa Ujumbe wa wafanyabiashara kutoka China, Bw. Lyu Xinhua, Balozi wa China nchini Mhe. Wang Ke, Mkurugenzi Mtendaji wa IPP Touchmate, Bw. Victor Tesha pamoja Msaidizi wa Dk. Mengi, Bw. Godfrey Bitesigirwe.
Balozi wa China nchini Mhe. Wang Ke akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Kiongozi wa Ujumbe wa wafanyabiashara kutoka China, Bw. Lyu Xinhua kutoa salamu wakati wa chakula cha mchana kilichoandaliwa Dr. Mengi kwa wawakilishi wa makampuni 17 kutoka China waliopo nchini kutafuta fursa za uwekezaji katika hafla fupi iliyofanyika Serena Hotel jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Dr. Reginald Mengi (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa IPP Touchmate, Bw. Victor Tesha (wa pili kulia) pamoja Msaidizi wa Dk. Mengi, Bw. Godfrey Bitesigirwe (kulia).
Kiongozi wa Ujumbe wa wafanyabiashara kutoka China, Bw. Lyu Xinhua akitoa salamu kwa niaba ya ujumbe huo wakati wa chakula cha mchana kilichoandaliwa Dr. Mengi kwa wawakilishi wa makampuni 17 kutoka China waliopo nchini kutafuta fursa za uwekezaji katika hafla fupi iliyofanyika Serena Hotel jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Dr. Reginald Mengi
Sehemu ya wafanyabiashara wawakilishi wa makampuni 17 kutoka China waliopo nchini kutafuta fursa za uwekezaji waliposhiriki hafla fupi ya chakula cha mchana kilichoandaliwa Dr. Mengi iliyofanyika Serena Hotel jijini Dar es Salaam.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Dk Mengi afungua milango ya ushirikiano na wawekezaji wa Kichina
yaani makala yote Dk Mengi afungua milango ya ushirikiano na wawekezaji wa Kichina Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Dk Mengi afungua milango ya ushirikiano na wawekezaji wa Kichina mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/dk-mengi-afungua-milango-ya-ushirikiano.html
0 Response to "Dk Mengi afungua milango ya ushirikiano na wawekezaji wa Kichina"
Post a Comment