Loading...
title : DC NAMTUMBO AIAGIZA TAKUKURU KUICHUNGUZA HALMASHAURI .
link : DC NAMTUMBO AIAGIZA TAKUKURU KUICHUNGUZA HALMASHAURI .
DC NAMTUMBO AIAGIZA TAKUKURU KUICHUNGUZA HALMASHAURI .

Kizigo aliyasema hayo hivi karibuni katika mkutano wa baraza la madiwani wilayani humo baada ya kubaini baraza la madiwani kutoridhika na taarifa ya mkaguzi wa ndani wa Halmashauri hiyo juu ya kubadilisha matumizi ya fedha shilingi milioni 950.
Taarifa ya mkaguzi wa ndani wa Halmashuri hiyo bwana John Mwingira ilidai Halmashuri hiyo imebadilisha matumizi ya fedha kiasi cha shilingi milioni 950 na kutumika kwa matumizi mengineyo tofauti na ilivyokusudiwa .
Aidha bwana Mwingira katika taarifa yake hiyo alidai kuwa fedha hiyo imetumika kwa nia njema lakini zinatakiwa kurudishwa katika shughuli iliyokusudiwa na serikali kwa kutumia mapato ya ndani ambayo kwa sasa yanasuasua.
Taarifa hiyo ilisema katika shilingi milioni 950 milioni 500 zilikuwa Ruzuku ya serikali zikiwa na lengo la kujenga Hospitali ya wilaya ambapo katika fedha hiyo milioni 200 zilibadilishwa matumizi na kumalizia zahanati saba viporo vya Halmashuri hiyo na kuanza kutumika na milioni 20 nazo zilibaki kujenga jengo moja katika Hospitali ya wilaya na milioni 156 zilipelekwa kukamilisha chumba cha upasuaji katika kituo cha afya lusewa katika mamlaka ya mji mdogo wa Lusewa.
Milioni 450 kati ya hizo milioni 950 zilipokelewa na Halmashuri hiyo kutoka bodi ya mikopo ya serikali za mitaa LGLB ambazo nazo zililenga kujenga soko zilibadilishwa matumizi na kulipia deni la vifaa vya viwandani milioni 214 zilizokopa Halmashuri hiyo na milioni 26 zilitumika kununulia mashine ya kukusanyia ushuru (POS)ishirini.
Hivyo makala DC NAMTUMBO AIAGIZA TAKUKURU KUICHUNGUZA HALMASHAURI .
yaani makala yote DC NAMTUMBO AIAGIZA TAKUKURU KUICHUNGUZA HALMASHAURI . Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DC NAMTUMBO AIAGIZA TAKUKURU KUICHUNGUZA HALMASHAURI . mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/dc-namtumbo-aiagiza-takukuru.html
0 Response to "DC NAMTUMBO AIAGIZA TAKUKURU KUICHUNGUZA HALMASHAURI ."
Post a Comment