Loading...
title : Dkt. Mwakyembe-Lugha ni Kielelezo cha Taifa
link : Dkt. Mwakyembe-Lugha ni Kielelezo cha Taifa
Dkt. Mwakyembe-Lugha ni Kielelezo cha Taifa
Na. Lorietha Laurence-WHUSM,Dodoma
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kuwa lugha ni kielelezo na sehemu muhimu ya utambulisho wa taifa lolote duniani. Hayo ameyasema jana Jijini Dodoma katika Hafla ya kuwatunuku vyeti vya utambuzi wataalamu 67 wa lugha ya Kiswahili waliofuzu mafunzo ya muda mfupi yaliyoandaliwa na Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA).
“Taifa lolote lisilo na utamaduni wake ni taifa mfu, na sisi tunajivunia kwa kuwa na utamaduni hai ikiwemo lugha yetu ya Kiswahili” alisema Dkt. Mwakyembe Aidha aliongeza kwa kueleza kuwa lugha ya Kiswahili ni kitambulisho cha utamaduni wa Mtanzania , kwa kuwa ndiyo lugha inayowaunganisha watu katika shughuli mbalimbali za Kijamii, Kisiasa na kiuchumi. Dkt. Mwakyembe anazidi kufafanua kuwa takribani lugha elfu sita (6000) huzungumzwa kila siku duniani ambapo lugha ya Kiswahili ni miongoni mwa lugha 10 zinazoongelewa kwa wingi.
“Mafunzo haya ni mwanzo tu mwa mambo mengi mazuri ambayo Wizara yangu imepanga kufanikisha na ukizingatia kampeni ya mwaka huu ya Uzalendo na Utaifa ina kauli mbiu inayohamasisha kukuza lugha yetu ambayo ni Kiswahili Utashi Wetu, Uhai Wetu” alisema Dkt. Mwakyembe.
Naye Kaimu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) Bibi.
Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akiongea na wataalamu wa lugha ya Kiswahili ( Hawapo katika picha), jana Jijini Dodoma katika halfa ya kuwatunuku vyeti vya utambuzi wataalamu 67 waliofuzu mafunzo ya muda mfupi yaliyoandaliwa na Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) jana Jijini Dodoma..
Mhitimu ambaye ni Mwalimu wa shule ya Sekondari Chikole ya Jijini Dodoma Bibi. Neema Mkobalo akisoma risala kwa mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (Wa tatu kulia) katika halfa ya kuwatunuku vyeti vya utambuzi wataalamu 67 wa lugha ya Kiswahili waliofuzu mafunzo ya muda mfupi yaliyoandaliwa na Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) jana Jijini Dodoma.
Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (Kulia) akimkabidhi cheti mmoja wa wahitimu wa mafunzo ya muda mfupi ya wataalamu wa lugha ya Kiswahili Mwalimu wa Shule ya Msingi Chikowa Bibi. Theresia Lejale jana Jijini Dodoma.
Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (Kulia) akimkabidhi cheti mmoja wa wahitimu wa mafunzo ya muda mfupi ya wataalamu wa lugha ya Kiswahili Mwalimu wa wa Shule ya Msingi Vikonje Bw. Emmanuel Mzumya jana Jijini Dodoma.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Dkt. Mwakyembe-Lugha ni Kielelezo cha Taifa
yaani makala yote Dkt. Mwakyembe-Lugha ni Kielelezo cha Taifa Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Dkt. Mwakyembe-Lugha ni Kielelezo cha Taifa mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/dkt-mwakyembe-lugha-ni-kielelezo-cha.html
0 Response to "Dkt. Mwakyembe-Lugha ni Kielelezo cha Taifa"
Post a Comment