Loading...

DKT. MWANJELWA AITAKA TAKUKURU KUHAKIKISHA INADHIBITI MIANYA YA RUSHWA

Loading...
DKT. MWANJELWA AITAKA TAKUKURU KUHAKIKISHA INADHIBITI MIANYA YA RUSHWA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa DKT. MWANJELWA AITAKA TAKUKURU KUHAKIKISHA INADHIBITI MIANYA YA RUSHWA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : DKT. MWANJELWA AITAKA TAKUKURU KUHAKIKISHA INADHIBITI MIANYA YA RUSHWA
link : DKT. MWANJELWA AITAKA TAKUKURU KUHAKIKISHA INADHIBITI MIANYA YA RUSHWA

soma pia


DKT. MWANJELWA AITAKA TAKUKURU KUHAKIKISHA INADHIBITI MIANYA YA RUSHWA

Serikali imeitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)  kuelekeza nguvu zaidi kuhakikisha mianya ya rushwa ndani ya taasisi za umma na jamii kwa ujumla inadhibitiwa ipasavyo ikiwa ni pamoja na kutowaonea haya wanaobainika kujihusisha na vitendo vya rushwa bila kujali vyeo vyao. Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati akifunga mkutano mkuu wa siku mbili wa mwaka wa viongozi wa TAKUKURU nchini uliofanyika katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa, jijini Dodoma.
Mhe. Mwanjelwa amesema, watumishi wote wa TAKUKURU wamekula kiapo na wamepewa dhamana ya kuzuia na kupambana na rushwa, hivyo wametakiwa kutomuogopa mtu yeyote anayejihusisha na rushwa na kumshughulikia ipasavyo kwa mujibu wa sheria.
Mhe. Mwanjelwa ameongeza kuwa, katika kutekeleza azma ya serikali kufikia uchumi wa kati wa viwanda, TAKUKURU ikiwa ni taasisi iliyopewa dhamana na serikali ya kupambana na rushwa, haina budi kudhibiti vitendo vya rushwa katika sekta zilizopewa kipaumbele katika Mkakati wa Kitaifa Dhidi ya Rushwa na Mpango wa Utekelezaji Awamu ya Tatu (NACSAP III).
Mhe. Mwanjelwa ameziainisha sekta zilizopewa kipaumbele, kuwa ni pamoja na sekta ya manunuzi ya umma, ukusanyaji wa mapato, maliasili na utalii, madini, gesi, afya, elimu na ardhi, hivyo TAKUKURU kuanzia ngazi ya wilaya inapaswa kutoa mchango kufikia uchumi wa kati wa viwanda. Aidha, Mhe. Mwanjelwa amerejea maelekezo ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) kwa TAKUKURU alipokuwa akifungua mkutano huo ya kuwataka wadhibiti mianya ya rushwa katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwakani ambapo nae amesisitiza vitendo vya rushwa vidhibitiwe kikamilifu kwani ni kikwazo cha upatikanaji wa viongozi wenye sifa na uadilifu.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na viongozi wa TAKUKURU nchini wakati akifunga mkutano mkuu wa mwaka wa siku mbili wa viongozi hao uliofanyika katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa, jijini Dodoma.
Viongozi wa TAKUKURU nchini wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati akifunga mkutano mkuu wa mwaka wa siku mbili wa viongozi hao uliofanyika katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa, jijini Dodoma.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala DKT. MWANJELWA AITAKA TAKUKURU KUHAKIKISHA INADHIBITI MIANYA YA RUSHWA

yaani makala yote DKT. MWANJELWA AITAKA TAKUKURU KUHAKIKISHA INADHIBITI MIANYA YA RUSHWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala DKT. MWANJELWA AITAKA TAKUKURU KUHAKIKISHA INADHIBITI MIANYA YA RUSHWA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/dkt-mwanjelwa-aitaka-takukuru.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "DKT. MWANJELWA AITAKA TAKUKURU KUHAKIKISHA INADHIBITI MIANYA YA RUSHWA"

Post a Comment

Loading...