Loading...
title : HATUNA MPANGO WA KUTOA SARAFU MPYA-PROFESA LUOGA
link : HATUNA MPANGO WA KUTOA SARAFU MPYA-PROFESA LUOGA
HATUNA MPANGO WA KUTOA SARAFU MPYA-PROFESA LUOGA
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania Profesa Florens Luoga amesema hawaoni sababu ya kubalisha sarafu na kwamba zilizopo zinatosha na wanataka ziwe nyingi zaidi kwa lengo la kuhakikisha noti zilizopo zinatumika kwa muda mrefu.
Profesa Florens ametoa kauli hiyo leo Mjini Dodoma wakati anajibu baadhi ya maswali ya waandishi wa habari za fedha na uchumi kabla ya kufunga semina ya mafunzo ya uandishi wa habari zinazohusu fedha na uchumi iliyoandaliwa na BoT.
Ambapo waandishi walitaka kufahamu kama Tanzania nayo itabadili sarafu yake kama ambavyo nchi ya Kenye imefanya kwa kutoa sarafu mpya ambapo amesema hakuna mpango huo kwa sasa."Tanzania tuna sarafu za kutosha na tunataka ziwe nyingi zaidi ili zitumike kwa wingi na lengo ni kuona noti zetu zinaishi muda mrefu zaidi.Kuhusu Kenya na uamuzi wa kubadili sarafu yao ni uamuzi wao na hauna tatizo kwenye uchumi wetu," amesema.
Hata hivyo amesema wakati Kenya imeamua kufanya uamuzi wa kutoa sarafu mpya tayari Jumuiya ya Afrika Mashariki imeshapitisha sheria ya Benki ya Afrika Mashariki na ifikapo mwaka 2024 nchi wanachama zinatakiwa kuwa na sarafu moja.Pia ametumia nafasi hiyo kuzungumzia ubora wa noti ya Tanzania ambayo asilimia 100 inatengenezwa kwa pamba , hivyo kuifanya kuwa imara zaidi kuliko Dola."Noti yetu ni imara sana na ukiwambia watu uimara wake ni zaidi ya Dola wanaweza wasiamini."
Gavana wa Benki Kuu Profesa Florens Luoga akifafanua jambo wakati anazungumza na waandishi wa habari za fedha na uchumi ambapo ametumia nafasi hiyo kuzungumzia sarafu ya Tanzania
Mkurugenzi wa BoT tawi la Dodoma Richard Wambali akitoa neno la shukrani kwa Gavana wa BoT Profesa Florens Luoga kabla ya kufunga mafunzo ya habari za fedha na uchumi kwa waandishi wa habari
Meneja wa Idara ya Uhusiano kwa umma na Itifaki kutoka BoT Zaria Mbeo akitoa majumuisho ya mafunzo ya habari za fedha na uchumi kwa Gavana BoT Profesa Florens Luoga
Hivyo makala HATUNA MPANGO WA KUTOA SARAFU MPYA-PROFESA LUOGA
yaani makala yote HATUNA MPANGO WA KUTOA SARAFU MPYA-PROFESA LUOGA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala HATUNA MPANGO WA KUTOA SARAFU MPYA-PROFESA LUOGA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/hatuna-mpango-wa-kutoa-sarafu-mpya.html
0 Response to "HATUNA MPANGO WA KUTOA SARAFU MPYA-PROFESA LUOGA"
Post a Comment