Loading...
title :
link :
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameushukuru na ameupongeza Uongozi wa Kampuni ya Simu Tanzania {TTCL} kwa Uzalendo wake inaojitolea wakati wote wa kuiunga mkono Serikali katika masuala ya kutunza Mazingira.
Alisema kitendo cha Kampuni hiyo kujitolea kujenga ukuta wa Mawe uliotumia Taaluma ya Kisasa kwa kuzuia athari ya Mmong’onyoko wa Ardhi katika eneo la Michakaeni Chake chake Pemba mbali ya kunusuru Mnara wao wa Mawasiliano lakini pia umesaidia kuepusha athari kwa Nyumba na Skuli iliyopo jirani.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa pongezi hizo baada ya kuukagua Ukuta huo wenye urefu wa Mita 14 ambao uko chini ya Mlima unaoonekana kuathirika mara kwa mara na Mvua za Masika za kila Mwaka hasa zile zilizonyesha Mwaka jana na kuleta athari kubwa.
Alisema ukuta huo kwa kiasi kikubwa umeweza kuleta Faraja kubwa kwa Wakaazi wanaouzunguuka Mlima wa hapo Michakaeni ambapo pia alizikumbusha Taasisi nyengine na Wananchi hapa Nchini waendelee kuchukuwa hadhari kukinga athari zinazoweza kuleta Mmong’onyoko.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliushauri Uongozi huo wa Kampuni ya Simu Tanzania {TTCL} kuendelea na mipango yao mengine ya kusaidia huduma za Kijamii na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iko tayari kuongeza nguvu katika kuona miradi hiyo inafanikiwa vyema.
Alisema TTCL ni Kampuni ya Kizalendo iliyoundwa kwa lengo la kutoa huduma bora kwa Wananchi kurahisishia kupata Mawasiliano ya uhakika yatakayoongeza chachu ya maendeleo yao ya kila siku.
Mapema Meneja wa Kampuni ya Simu Tanzania kwa upande wa Pemba Nd. Khamis Ishaq Ngwali alisema Ujenzi wa ukuta huo wa kuzuia Mmong’onyoko wa Ardhi umekuja kufuatia mvua kubwa za Mwaka jana zilizoathiri eneo hilo.
Nd. Ishaq alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba Uongozi wa TTCL kupitia Bodi ya Kampuni hiyo ulifikia hatua ya kujenga ukuta huo ili kunusuru uharibikaji wa mazingira katika eneo hilo lililozunguukwa na Majengo ya huduma.
Alisema kutokana na mazingira halisi ya eneo hilo lilivyo likiwa na Mlima TTCL ina malengo ya kuendelea na ujenzi wa ukuta huo kwa awamu Mbili zijazo ili kupafanya pawe salama mahali hapo.
Meneja huyo wa TTCL Pemba alifahamisha kwamba jumla ya Shilingi Milioni 39,344,000,000/- zimetumika katika ujenzi wa ukuta huo uliotumia Mawe na Waya lakini gharama hizo zingepanda zaidi iwapo wangeamua kutumia ujenzi wa zege
Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alitembelea Hospitali ya Rufaa ya Abdallah Mzee Mkoani kuangalia huduma za Afya zinazotolewa kwa Wananchi pamoja na kuona changamoto zinazowakabili watendaji wa Hospitali hiyo.
Balozi Seif aliuagiza Uongozi wa Hospitali hiyo kukaa na Afisa Mdhamini pamoja na Uongozi wa juu wa Wizara ya Afya kuainisha changamoto zinazowakabili ikiwemo vifaa vilivyoharibika ili Wizara izifanyie kazi.
Alisema haipendezi hata kidogo kuona kwamba Mshirika mkubwa wa Maendeleo ya Zanzibar Nchi ya China inajikita kusaidia gharama za uendelezaji miradi mbali mbali ikiwemo Hospitali na kutumia fedha za Walipa Kodi wake lakini muda mfupi baadae miradi hiyo inazorota au kufa kabisa.
Alisema vitendo kama hivyo vinapotokea mbali ya kuitia hasara kubwa Serikali pamoja na kuwakosesha huduma Wananchi lakini pia huwavunja moyo Washirika hao wanapoamua kusaidia Maendeleo.
Hivyo makala
yaani makala yote
Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/makamu-wa-pili-wa-rais-wa-zanzibar_11.html
0 Response to " "
Post a Comment