Loading...

MAMA MARIA NYERERE AZUNGUMZA NA NDUGU BASHIRU ,AMTAKA ASONGE MBELE KUREJESHA CHAMA KWENYE MISINGI

Loading...
MAMA MARIA NYERERE AZUNGUMZA NA NDUGU BASHIRU ,AMTAKA ASONGE MBELE KUREJESHA CHAMA KWENYE MISINGI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MAMA MARIA NYERERE AZUNGUMZA NA NDUGU BASHIRU ,AMTAKA ASONGE MBELE KUREJESHA CHAMA KWENYE MISINGI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MAMA MARIA NYERERE AZUNGUMZA NA NDUGU BASHIRU ,AMTAKA ASONGE MBELE KUREJESHA CHAMA KWENYE MISINGI
link : MAMA MARIA NYERERE AZUNGUMZA NA NDUGU BASHIRU ,AMTAKA ASONGE MBELE KUREJESHA CHAMA KWENYE MISINGI

soma pia


MAMA MARIA NYERERE AZUNGUMZA NA NDUGU BASHIRU ,AMTAKA ASONGE MBELE KUREJESHA CHAMA KWENYE MISINGI

Mjane wa Mwalimu Nyerere Mwenyekiti wa Kwanza wa CCM na Rais wa kwanza wa Tanzania, Mama Maria Nyerere amekutana na kuwa na mazungumzo na Ndugu Bashiru Ally Kakurwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mama Maria ametumia mkutano huu kumpongeza Ndugu Katibu Mkuu kwa juhudi kubwa ambazo anaendelea kuzifanya za kumsaidia Ndugu John Pombe Joseph Magufuli Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kukirejesha Chama na Serikali kwenye misingi ambayo baba wa Taifa aliisimamia.

Mama Maria kwa umahususi na kwa kupitia kwa Ndugu Bashiru amempongeza Ndugu Magufuli kwa kazi nzuri ya ujenzi wa vituo vya afya zaidi ya 200 kote nchini Tanzania ndani ya kipindi kifupi cha miaka miwili, vituo ambayo vina huduma ya afya timilifu (comprehensive health care). Mama Maria ameeleza vituo hivi vitakuwa mkombozi wa upatikanaji wa huduma za afya hasa kwa mama, watoto na wazee. Katika Mkutano huo Mama Maria ametoa wito kwa CCM kuendelea kuisimamia Serikali na kuimarisha lishe bora kwa watoto, watu wazima na umma ili kujenga Taifa imara na la watu wenye nguvu ya kuendelea kuchapa kazi sambamba na kauli mbiu ya Rais Magufuli ya Hapa Kazi Tu!
Akipokea pongezi hizo Ndugu Bashiru Ally, amemshukuru Mama Maria kwa kuendelea kutujali, kutukumbusha, kutushauri na kutuombea kila anapopata nafasi. Ndugu Bashiru amemjulisha Mama Maria kwamba tarehe 17 na 18 Desemba kutafanyika vikao vya Uongozi vya Taifa, Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa na Halmashauri Kuu ya Taifa ambapo serikali zote mbili ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zitatoa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa Mwaka 2015 – 2020.

Huu ni muendelezo wa ziara na mazungumzo ya Ndugu Bashiru Ally na viongozi, makada na wanachama wa CCM ili kupokea ushauri, kubadilishana nao uelewa, mipango, mikakati na taarifa za ujenzi wa Chama.


Hivyo makala MAMA MARIA NYERERE AZUNGUMZA NA NDUGU BASHIRU ,AMTAKA ASONGE MBELE KUREJESHA CHAMA KWENYE MISINGI

yaani makala yote MAMA MARIA NYERERE AZUNGUMZA NA NDUGU BASHIRU ,AMTAKA ASONGE MBELE KUREJESHA CHAMA KWENYE MISINGI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MAMA MARIA NYERERE AZUNGUMZA NA NDUGU BASHIRU ,AMTAKA ASONGE MBELE KUREJESHA CHAMA KWENYE MISINGI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/mama-maria-nyerere-azungumza-na-ndugu.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MAMA MARIA NYERERE AZUNGUMZA NA NDUGU BASHIRU ,AMTAKA ASONGE MBELE KUREJESHA CHAMA KWENYE MISINGI"

Post a Comment

Loading...