Loading...

MAMLAKA YA HALI YA HEWA YAAMUA KUTAJA SABABU ZA KUONGEZEKA KWA JOTO NCHINI

Loading...
MAMLAKA YA HALI YA HEWA YAAMUA KUTAJA SABABU ZA KUONGEZEKA KWA JOTO NCHINI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MAMLAKA YA HALI YA HEWA YAAMUA KUTAJA SABABU ZA KUONGEZEKA KWA JOTO NCHINI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MAMLAKA YA HALI YA HEWA YAAMUA KUTAJA SABABU ZA KUONGEZEKA KWA JOTO NCHINI
link : MAMLAKA YA HALI YA HEWA YAAMUA KUTAJA SABABU ZA KUONGEZEKA KWA JOTO NCHINI

soma pia


MAMLAKA YA HALI YA HEWA YAAMUA KUTAJA SABABU ZA KUONGEZEKA KWA JOTO NCHINI

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania(TMA) imeamua kutoa ufafanuzi kwa jamii ya Watanzania kuhusu hali ya ongezekeo la joto katika baadhi ya maeneo hapa nchini huku ikifafanua kwenye baadhi ya mikoa joto limefikia asilimia 34.

Taarifa ya TMA kwa vyombo vya habari ambayo imetoa leo jijini Dar es Salaam imesema kwa kawaida kipindi cha Oktoba hadi Machi kila mwaka jua la utosi linakuwa katika maeneo ya kizio cha kusini mwa dunia na Tanzania ikiwa ni moja ya nchi zilizopo katika kizio cha kusini, huwa na hali ya joto kali katika maeneo mengi ikilinganishwa na miezi mingine. 

"Hapa nchini, vipindi vya jua la utosi vinafikia kilele kati ya mwishoni mwa Novemba na Desemba wakati jua la utosi likiwa linaelekea kusini (Tropiki ya Kaprikoni) na hali hiyo hujirudia tena Februari wakati jua la utosi likiwa linaelekea kaskazini (Tropiki ya Kansa). Jua la utosi huambatana na hali ya Joto kali kwa sababu kipindi hicho ndipo uso wa dunia katika eneo tajwa huwa karibu zaidi na jua kuliko maeneo mengine. Hali hii hushuhudiwa zaidi kunapokuwepo na upungufu wa mvua ambazo zingesaidia katika kupunguza hali ya joto katika kipindi husika,"imesema taarifa hiyo ya TMA.

Imefafanua wastani wa joto kwa Novemba na Desemba ni nyuzi joto 31.5 kwa mikoa ya Dar es Salaam, Tanga na visiwa vya Unguja na Pemba. Hata hivyo, mpaka kufika mwishoni mwa Novemba 2018 joto limeshafika nyuzi joto 34. Katika baadhi ya maeneo hapa nchini ikiwemo mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Morogoro, Dar es salaam, Pwani pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba ambapo msimu wa mvua za Vuli unaendelea kukumbwa na mtawanyiko hafifu wa mvua hali ya fukuto inachangia katika hali ya joto japo vipimo vya nyuzi joto katika baadhi ya maeneo hayo ni vya wastani.

Imeongeza kuwa vipindi hivyo vya joto kali vinatarajiwa kupungua kadiri mtawanyiko wa mvua za vuli utakavyoimarika Desemba mwaka huu wa 2018 huku ikifafanua kuwa hata hivyo ikizingatiwa kuwa hali ya joto inatarajiwa kujirudia tena Februari 2019, wakati wa kipindi cha pili cha jua la utosi. Aidha, taarifa za mwenendo wa joto, zinaendelea kutolewa katika 

utabiri wa kila siku na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania na kwamba wanatoa mwito kwa wananchi kuendelea kufuatilia taarifa hizo na kuchukua hatua stahiki kila inapobidi.


Hivyo makala MAMLAKA YA HALI YA HEWA YAAMUA KUTAJA SABABU ZA KUONGEZEKA KWA JOTO NCHINI

yaani makala yote MAMLAKA YA HALI YA HEWA YAAMUA KUTAJA SABABU ZA KUONGEZEKA KWA JOTO NCHINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MAMLAKA YA HALI YA HEWA YAAMUA KUTAJA SABABU ZA KUONGEZEKA KWA JOTO NCHINI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/mamlaka-ya-hali-ya-hewa-yaamua-kutaja.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MAMLAKA YA HALI YA HEWA YAAMUA KUTAJA SABABU ZA KUONGEZEKA KWA JOTO NCHINI"

Post a Comment

Loading...