Loading...

MEMBE AIBUKA KANISANI KRISMASI

Loading...
MEMBE AIBUKA KANISANI KRISMASI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MEMBE AIBUKA KANISANI KRISMASI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MEMBE AIBUKA KANISANI KRISMASI
link : MEMBE AIBUKA KANISANI KRISMASI

soma pia


MEMBE AIBUKA KANISANI KRISMASI









Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Serikali ya awamu ya nne, Bernard Membe amekuwa miongoni mwa waumini wa dini ya kikristo walioshiriki ibada ya Krismasi katika kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam.

Membe ambaye aliwahi kuwa mbunge wa Mtama, ameshiriki misa hiyo leo Jummane Desemba 25, 2018 iliyoongozwa na Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Eusebius Nzigilwa.

Katika ibada hiyo, Membe ambaye hivi karibuni alizua gumzo kati yake na Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally, alionekana kwenye safu ya mbele akiwa amevaali suti ya rangi nyeusi.

Membe alikuwa gumzo hivi karibuni baada ya Dk Bashiru kutamka hadharani kuwa waziri huyo wa zamani anakwamisha mikakati ya urais ya 2020.

Ibada hiyo ilikuwa ya pili na ilianza saa nne, baada ya ile asubuhi kuhudhuriwa na mke wa Rais Janeth Magufuli.

Akitoa mahubiri katika ibada hiyo, Askofu Nzigilwa amesema Sikukuu ya Krismasi ina neema ya matunda manne na ni vyema waumini wa dini wakayazingatia.

Amesema matunda hayo kuwa ni upatanisho, furaha, umoja na amani na kusema ni vyema waumini wa dini wakayatilia mkazo wakati wakisherehekea Krismasi.

“Tunaishi dunia yenye misuguano, kuna watu hawaongei katika maeneo mbalimbali ikiwemo ya kazi tena wengine pia wanaishi nyumba moja halafu tunasema tunasheherekea Krismasi, sikukuu gani hiyo wakati hakuna upatanisho?” Alihoji Askofu Nzigilwa.



Hivyo makala MEMBE AIBUKA KANISANI KRISMASI

yaani makala yote MEMBE AIBUKA KANISANI KRISMASI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MEMBE AIBUKA KANISANI KRISMASI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/membe-aibuka-kanisani-krismasi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MEMBE AIBUKA KANISANI KRISMASI"

Post a Comment

Loading...