Loading...

MFANYABIASHARA JIJINI ARUSHA HANSPAUL AHUKUMIWA KULIPA FAINI YA MILIONI 60 AU KWENDA JELA MIAKA 2

Loading...
MFANYABIASHARA JIJINI ARUSHA HANSPAUL AHUKUMIWA KULIPA FAINI YA MILIONI 60 AU KWENDA JELA MIAKA 2 - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MFANYABIASHARA JIJINI ARUSHA HANSPAUL AHUKUMIWA KULIPA FAINI YA MILIONI 60 AU KWENDA JELA MIAKA 2, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MFANYABIASHARA JIJINI ARUSHA HANSPAUL AHUKUMIWA KULIPA FAINI YA MILIONI 60 AU KWENDA JELA MIAKA 2
link : MFANYABIASHARA JIJINI ARUSHA HANSPAUL AHUKUMIWA KULIPA FAINI YA MILIONI 60 AU KWENDA JELA MIAKA 2

soma pia


MFANYABIASHARA JIJINI ARUSHA HANSPAUL AHUKUMIWA KULIPA FAINI YA MILIONI 60 AU KWENDA JELA MIAKA 2


NA Vero Ignatus -ARUSHA

MFANYABIASHARA maarufu Jijini Arusha,Kamaljit Hanspaul (58), anayejishughulisha na shughuli mbalimbali na wenzake watatu wamehukumiwa kulipa faini ya Sh Milioni 60 au kwenda jela miaka miwili kila mmoja baada ya kukutwa na hatia ikiwemo kuajiri wafanyakazi watatu raia wa kigeni kufanya kazi nchini bila vibali.

Mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha,washitakiwa wengine ambao uraia uko kwenye mabano Vemula Shivakumar, (27), (India) Sathasivam Krishanth, (29) (India) na Ralph Leonard, (54), (Ujerumani),ambapo watuhumiwa wote wanne walikiri kutenda makosa hayo mwanzoni mwa wiki.

Akisoma hukumu hiyo jana,Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo,Niku Mwakatobe,alisema Mahakama hiyo imemtia hatiani Hanspaul katika mashitaka matatu ambayo ni kuajiri raia watatu wa kigeni ambao hawakuwa na vibali vya kufanya kazi nchini.

Alisema baada ya mshitakiwa huyo kukiri mashitaka hayo Mahakama inamtoza faini ya Sh Milioni 10 kila kosa au kifungo cha miaka miwili,huku washitakiwa wengine wakitozwa faini ya Sh Milioni 10 kila mmoja au kifungo cha miaka miwili baada ya kukutwa na hatia ya kufanya kazi nchini bila vibali.

Washitakiwa wote wanne waliachiwa huru baada ya kulipa faini hiyo Sh Milioni 60,ambapo katika uamuzi wake,Hakimu Niku aliwataka raia hao iwapo wanataka kuendelea kufanya kazi hapa nchini,wafuate taratibu na sheria zilizowekwa.Katika shauri hilo jamhuri ilikuwa ikiwakilishwa na Wakili Khalili Nuda huku utetezi ukiwakilishwa na Wakili Salumi Mushi,ambaye aliiomba Mahakama ipunguze adhabu ikizingatiwa ni mara ya kwanza kwa washitakiwa hao kukutwa na hatia na kuwa washitakiwa watatu ambao ni raia wa kigeni walishaaanza taratibu za kufuatilia vibali vya kufanya kazi nchini.

Naye Wakili Nuda aliiomba Mahakama licha ya watuhumiwa wote kutokuwa na rekodi ya kukutwa na hatia,wanaomba Mahakama iwaadhibu kwa mujibu wa sheria na kuomba iwaagize iwapo wanataka kuendelea kufanya kazi hapa nchini wafuate sheria na taratibu.

Awali katika shauri hilo namba 389 la mwaka huu kabla ya kusomewa hukumu hiyo washitakiwa hao walisomewa maelezo ya awali,ambapo Wakili Nuda alidai mshitakiwa wa kwanza,aliwaajiri Shivakumar, Krishanth na Ralph kufanya kazi kama washauri kwenye kampuni yake ya HansPaul Automechs iliyopo maeneo ya Njiro jijini hapa wakati akijua hawana vibali vya kufanya kazi nchini.


Hivyo makala MFANYABIASHARA JIJINI ARUSHA HANSPAUL AHUKUMIWA KULIPA FAINI YA MILIONI 60 AU KWENDA JELA MIAKA 2

yaani makala yote MFANYABIASHARA JIJINI ARUSHA HANSPAUL AHUKUMIWA KULIPA FAINI YA MILIONI 60 AU KWENDA JELA MIAKA 2 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MFANYABIASHARA JIJINI ARUSHA HANSPAUL AHUKUMIWA KULIPA FAINI YA MILIONI 60 AU KWENDA JELA MIAKA 2 mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/mfanyabiashara-jijini-arusha-hanspaul.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MFANYABIASHARA JIJINI ARUSHA HANSPAUL AHUKUMIWA KULIPA FAINI YA MILIONI 60 AU KWENDA JELA MIAKA 2"

Post a Comment

Loading...