Loading...
title : MKUTANO KAZI BAINA YA WADAU WA MAENDELEO, MAAFISA WA SERIKALI NA WATENDAJI TASAF WAMALIZIKA KWA MAFANIKIO JIJINI DAR
link : MKUTANO KAZI BAINA YA WADAU WA MAENDELEO, MAAFISA WA SERIKALI NA WATENDAJI TASAF WAMALIZIKA KWA MAFANIKIO JIJINI DAR
MKUTANO KAZI BAINA YA WADAU WA MAENDELEO, MAAFISA WA SERIKALI NA WATENDAJI TASAF WAMALIZIKA KWA MAFANIKIO JIJINI DAR
Na Estom Sanga-DSM
Mkutano wa Wadau wa Maendeleo ,Maafisa wa Serikali na Watendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF uliojadili kwa kina utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ambao unatekelezwa na Serikali kupitia TASAF umemalizika jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo ambao hufanyika kila baada ya miezi sita , umefanyika kufuatia ziara ya washiriki hao katika wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza na Unguja ambako walikutana na Walengwa wa Mpango huo na kujionea namna Walengwa wanavyoendelea kunufaika na huduma zinazotolewa na Mpango huo kuboresha maisha yao.
Miongoni mwa mambo yaliyofanywa katika mkutano huo ni pamoja na kuweka mkakati wa utekelezaji wa awamu ya pili ya Mpangowa Kunusuru Kaya Maskini inayotarajiwa kuanza Mwezi Aprili hapo mwakani ambayo italenga zaidi katika kuwashirikisha Walengwa kufanyakazi za maendeleo kwenye maeneo yao na kisha kulipwa ujira.
Akizungumza na Washiriki wa Mkutano huo Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF,Bw. Ladislaus Mwamanga ametoa wito maalumu kwa wadau na maafisa wa Mfuko huo kufanya kazi kwa bidii na kuweka mbele maslahi ya taifa ili lengo la serikali la kuwapunguzia kero ya umaskini wananchi liweze kufikiwa kwa ufanisi.
Bwana Mwamanga amesema utekelezaji na mafanikio ya Mpango huo unategemea kwa kiwango kikubwa jitihada za pamoja hasa ikizingatiwa kuwa wananchi wanaolengwa ni wale ambao kwa kiwango kikubwa wamekuwa wakiishi katika hali ya umaskinina wengine kukata tamaa jambo ambalo amesema linapaswa kukabiliwa kwa nguvu za pamoja.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhFknn9X1xqipNyl7o0tIvqTmEu3opLwmtIuYYb2xUqou1NZJYcriLuPqNE3pNdpznDHfSMkoxBt5SpGyuuvCuChDDbEwABtIUkuUufNQ0A5lI1Jzoh1dKwg8iwagi8NhM_AGvI76FX9cuQ/s640/New+Picture+%25284%2529.png)
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Bw. Ladslaus Mwamanga (katikati) akiongoza mkutano wa Wadau wa Maendeleo, Maafisa wa Serikali na TASAF kwenye ukumbi wa Mfuko huo jijini Dar es Salaam.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg4pPuIVt2-rPrISGVBP3smvdKG1xuc9eg-Wg643mbWBWfLgZAzK9Bgjku41fEEHqndX2AgJJOPIZe9HyWg373HBPBzUTBHtnbpHO7HpMTd8IAhq-y1Siq36-Rf-5xWoLjm0Vi6UBavYWMX/s640/New+Picture.png)
Baadhi ya Washiriki wa Mkutano wa Wadau ,Serikali na TASAF wakiwa kwenye ukumbi wa Mikutano wa TASAF jijini DSM katika mkutano uliojadili utekelezaji wa Shughuli za Mfuko huo na maandalizi ya awamu ya pili ya Mpango huo inayotarajiwa kuanza hapo mwakani.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhdByIHgS6Ij2IH2sPHJfY90wU29N-7k6Ne_PcDErKqjDgeUbJDHd8NnZP8w69WVvXQ5DkiRzND9cfB-KDDV15d_e51f0kT1ktGQMN72JEiqyLhP_GRTMZeurg2u4yV-s78WRkrMk52G8A0/s640/New+Picture+%25281%2529.png)
Mmoja wa Watumishi wa TASAF,Shadrack Mziray akiwasilisha taarifa kwenye Mkutano wa Wadau ,serikali na TASAF jijini Dar es salaam.
Picha ya juu na chini menejimenti ya TASAF na ile ya Benki ya Dunia hapa nchini wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wa TASAF, Serikali Na Wadau wa Maendeleo baada kuhudhuria mkutano wao wa pamoja jijini Dar es salaam.
Hivyo makala MKUTANO KAZI BAINA YA WADAU WA MAENDELEO, MAAFISA WA SERIKALI NA WATENDAJI TASAF WAMALIZIKA KWA MAFANIKIO JIJINI DAR
yaani makala yote MKUTANO KAZI BAINA YA WADAU WA MAENDELEO, MAAFISA WA SERIKALI NA WATENDAJI TASAF WAMALIZIKA KWA MAFANIKIO JIJINI DAR Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MKUTANO KAZI BAINA YA WADAU WA MAENDELEO, MAAFISA WA SERIKALI NA WATENDAJI TASAF WAMALIZIKA KWA MAFANIKIO JIJINI DAR mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/mkutano-kazi-baina-ya-wadau-wa.html
0 Response to "MKUTANO KAZI BAINA YA WADAU WA MAENDELEO, MAAFISA WA SERIKALI NA WATENDAJI TASAF WAMALIZIKA KWA MAFANIKIO JIJINI DAR"
Post a Comment