Loading...
title : MGALU ACHANGIA MIFUKO YA SARUJI UJENZI WA OFISI MBILI ZA CCM KIBAHA VIJIJINI
link : MGALU ACHANGIA MIFUKO YA SARUJI UJENZI WA OFISI MBILI ZA CCM KIBAHA VIJIJINI
MGALU ACHANGIA MIFUKO YA SARUJI UJENZI WA OFISI MBILI ZA CCM KIBAHA VIJIJINI
NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA VIJIJINI
MBUNGE wa viti maalum mkoani Pwani, Subira Mgalu ameunga mkono jitihada za ujenzi wa ofisi ya Chama Cha Mapinduzi kata ya Mtongani na Mlandizi kwa kutoa mifuko ya saruji 40 yenye thamani ya zaidi ya laki sita.
Kati ya mifuko hiyo amechangia mifuko ya saruji 20 kwa kata ya Mtongani na mingine 20 kwenye kata ya Mlandizi . Subira alitoa mifuko hiyo ya saruji wakati alipokutana na baadhi ya viongozi wa chama ikiwa ni moja ya kazi za kichama. Alieleza hatochoka kushiriki kusaidiana kutatua changamoto zilizopo kichama na serikali.
“Ni wakati wa chama kukiimarisha kwa kujenga na kukarabati ofisi zetu, kuongeza vitendea kazi kwakuwa CCM mpya inajengwa lazima kwenda na wakati “alieleza Subira. Hata hivyo Subira aliwataka ,wanawake wasikate tamaa wathubutu kujitokeza kugombea nyadhifa mbalimbali.
“Tukaemkao wa kula sasa, tunaelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu, tusiogope, wanawake tujiamini “alifafanua Subira. Nae diwani wa kata ya Mlandizi Ephrasia Kadala, alisema Hili ulilolitenda leo ni kubwa kwa wanaCCM na wananchi kijumla, hivyo aliwaomba wadau wengine kujitolea kushirikiana ili kumaliza kama sio kuzitatua kero za zinazowakabili kichama”
Katibu wa Jumuiya ya wanawake (UWT) Kibaha Vijijni Janeth Mnyaga alimshukuru mbunge huyo kuwa bega kwa bega kushiriki nao kwenye shughuli za jumuiya na chama. Wakati huo huo Subira alitembelea kituo cha afya Mlandizi kujionea hali ya upanuzi wa majengo kwa gharama ya sh. Milioni 400 ambazo zimetolewa na serikali.
MBUNGE wa viti maalum mkoani Pwani, Subira Mgalu (wa kwanza kushoto) wakati alipokwenda kutembelea kituo cha afya Mlandizi kujionea hali ya ujenzi wa upanuzi wa kituo hicho ukiendelea, wa kwanza kulia mwenye kofia ni mbunge wa jimbo la Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa.
MBUNGE wa viti maalum mkoani Pwani, Subira Mgalu (wa kwanza kushoto) akipewa mkono wa pongezi na mmoja wa viongozi wa CCM kata ya Mtongani. (Picha na Mwamvua Mwinyi)
Hivyo makala MGALU ACHANGIA MIFUKO YA SARUJI UJENZI WA OFISI MBILI ZA CCM KIBAHA VIJIJINI
yaani makala yote MGALU ACHANGIA MIFUKO YA SARUJI UJENZI WA OFISI MBILI ZA CCM KIBAHA VIJIJINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MGALU ACHANGIA MIFUKO YA SARUJI UJENZI WA OFISI MBILI ZA CCM KIBAHA VIJIJINI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/mgalu-achangia-mifuko-ya-saruji-ujenzi.html
0 Response to "MGALU ACHANGIA MIFUKO YA SARUJI UJENZI WA OFISI MBILI ZA CCM KIBAHA VIJIJINI"
Post a Comment