Loading...
title : MKUU WA MKOA WA SIMIYU APEWA PONGEZI NA TBF ' MTAKA BASKETBALL TAIFA CUP'
link : MKUU WA MKOA WA SIMIYU APEWA PONGEZI NA TBF ' MTAKA BASKETBALL TAIFA CUP'
MKUU WA MKOA WA SIMIYU APEWA PONGEZI NA TBF ' MTAKA BASKETBALL TAIFA CUP'
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Mashindano ya Kombe la Taifa la Kikapu Tanzania (Mtaka Basketball Taifa Cup 2018) yamemalizika katika viwanja vya Halmashauri ya mji wa Bariadi, Jumapili 23 Dec, 2018 ambapo timu ya mkoa wa Dar es Salaam imeshinda Mwanza 78 kwa 75 na kutwaa kombe hilo.
Katika mashindano hayo mshindi wa pili ni Mwanza, wa tatu Shinyanga na wa nne ni Arusha. Zawadi za vikombe, medali na tuzo zilitolewa kwa washindi, wachezaji nyota wa michuano hii na kila timu, mwalimu na mchezaji aliyeshiriki alipewa cheti cha ushiriki.
Mashindano hayo yalifunguliwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mkata, 17Dec, 2018 na yamefungwa na Rais wa Shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania (TBF) Ndg. Phares Magesa tarehe 23 Dec 2018.
Shirikisho la Mpira wa Kikapu Nchini (TBF) limetoa shukrani nyingi kwa kazi nzuri iliyofanywa na Mkoa wa Simiyu chini ya uongozi wa Mkuu wa Mkoa Anthony Mtaka, Katibu Tawala Jumanne Sagini, Mkurugenzi wa mji wa Bariadi, Afisa michezo wa mkoa wa Simiyu, Afisa Vijana wa Mkoa wa Simiyu, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Simiyu pamoja na watendaji wote wa idara mbalimbali za Mkoa na wananchi wa Simiyu kwa ujumla kwa kufanikisha mashindano haya.
Licha ya mkoa huu kuwa ni mchanga ila kupitia jitihada za Viongozi hao na wadau walioko Simiyu wameweza kujenga uwanja mzuri wa kisasa wa kikapu ambao utaendelea kutumika kukuza vipaji vya kikapu mkoani hapa, na pia wameweza kuzihudumia na kuzikarimu vizuri timu zote zikizofika katika Mashindano haya.
TBF imekubali ombi la Mkoa huu kuandaa tena mashandano haya mwaka ujao ambapo yatafanyika Dec 2019 ambapo yataboreshwa zaidi kiufadhili na kimiundombinu ili kuwezesha timu za mikoa yote Tanzania Bara na Visiwani ziweze kushiriki.
Hivyo makala MKUU WA MKOA WA SIMIYU APEWA PONGEZI NA TBF ' MTAKA BASKETBALL TAIFA CUP'
yaani makala yote MKUU WA MKOA WA SIMIYU APEWA PONGEZI NA TBF ' MTAKA BASKETBALL TAIFA CUP' Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MKUU WA MKOA WA SIMIYU APEWA PONGEZI NA TBF ' MTAKA BASKETBALL TAIFA CUP' mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/mkuu-wa-mkoa-wa-simiyu-apewa-pongezi-na.html
0 Response to "MKUU WA MKOA WA SIMIYU APEWA PONGEZI NA TBF ' MTAKA BASKETBALL TAIFA CUP'"
Post a Comment