Loading...

NAIBU WAZIRI OLE NASHA ASHIRIKI ‘MSARAGAMBO’ WILAYANI SAME

Loading...
NAIBU WAZIRI OLE NASHA ASHIRIKI ‘MSARAGAMBO’ WILAYANI SAME - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa NAIBU WAZIRI OLE NASHA ASHIRIKI ‘MSARAGAMBO’ WILAYANI SAME, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : NAIBU WAZIRI OLE NASHA ASHIRIKI ‘MSARAGAMBO’ WILAYANI SAME
link : NAIBU WAZIRI OLE NASHA ASHIRIKI ‘MSARAGAMBO’ WILAYANI SAME

soma pia


NAIBU WAZIRI OLE NASHA ASHIRIKI ‘MSARAGAMBO’ WILAYANI SAME


Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha ameshiriki ‘msaragamo’ wa ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Ruvu iliyoko Kata ya Ruvu Darajani Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro.

Mheshimiwa Ole Nasha ameshiriki ujenzi huo na Wananchi wa Kijiji cha Ruvu Darajani wakati wa ziara ya kukagua miradi ya Elimu katika Wilaya ya Same ambapo amewataka wananchi kuendeleza jitihada hizo ili kuweza kuweka mazingira mazuri ya wanafunzi kusoma.

Kufuatia jitihada hizo za Wananchi Naibu Waziri Ole Nasha kupitia Wizara yake ameahidi kujenga vyumba viwili vya madarasa, mabweni mawili na matundu ya vyoo katika shule ya msingi Ruvu ikiwa ni kuunga mkono juhudi ambazo wananchi wa kijiji cha Ruvu Darajani wameonesha lakini pia kuwezesha wanafunzi kutulia shuleni na kusoma.

“Serikali ikiona eneo ambalo wananchi wameanza na wana hamasa kubwa ya kujiletea maendeleo haiwezi kusita kuja kusaidia, Wilaya ya Same mmeonesha mfano kupitia utaratibu wenu wa msaragambo tunaunga mkono jitihada hizo kwa kuwajengea vyumba vya madarasa, mabweni na matundu ya vyoo,” aliongeza Naibu Waziri Ole Nasha.

Aidha Naibu Waziri huyo amewataka wananchi wa Kijiji cha Ruvu Darajani ambao wanajihusisha na shughuli za ufugaji kutotumia watoto kuchunga mifugo badala yake kuhakikisha wanatumia fursa ya Elimu bure kuwaandikisha watoto wote wenye umri wa kuanza shule.

Awali Mkuu wa Wilaya ya Same Rosemary Staki alimweleza Naibu Waziri wa Elimu kuwa changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Ruvu imetokana na ongezeko la Wanafunzi waliohamishiwa shule hiyo kutokana na shule walizokuwa wakisoma miundombinu yake kuathiriwa na mafuriko yaliyotokana na mvua za masika zilizonyesha mwaka huu.

Katika ziara hiyo Naibu Waizri Ole Nasha pia alitembelea shule ya Sekondari Makanya, Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Same na Shule ya Sekondari Same ambapo ameridhishwa na namna ukarabati ulivyofanyika katika shule hiyo kongwe.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akishiriki ‘Msaragambo’ wa ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya Msingi Ruvu iliyoko Kata ya Ruvu Darajani Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro alipofanya ziara kukagua miradi ya Elimu inayotekelezwa katika Wilaya hiyo. 
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akikagua ukarabati wa miundombinu uliofanyika katika Shule ya Sekondari Same iliyoko Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro. Ameridhishwa na namna ukarabati huo ulivyofanyika na kuwataka kutunza miundombinu hiyo ili iweze kutumika kwa muda mrefu.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ruvu Darajani Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro. Amewataka kutumia fursa ya Elimu bure kuhakikisha wanaandikisha watoto wote wenye umri wa kuanza shule. 


Hivyo makala NAIBU WAZIRI OLE NASHA ASHIRIKI ‘MSARAGAMBO’ WILAYANI SAME

yaani makala yote NAIBU WAZIRI OLE NASHA ASHIRIKI ‘MSARAGAMBO’ WILAYANI SAME Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala NAIBU WAZIRI OLE NASHA ASHIRIKI ‘MSARAGAMBO’ WILAYANI SAME mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/naibu-waziri-ole-nasha-ashiriki.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "NAIBU WAZIRI OLE NASHA ASHIRIKI ‘MSARAGAMBO’ WILAYANI SAME"

Post a Comment

Loading...