Loading...

RADA MPYA KUONGEZA USALAMA WA ANGA NCHINI - TCAA

Loading...
RADA MPYA KUONGEZA USALAMA WA ANGA NCHINI - TCAA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa RADA MPYA KUONGEZA USALAMA WA ANGA NCHINI - TCAA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : RADA MPYA KUONGEZA USALAMA WA ANGA NCHINI - TCAA
link : RADA MPYA KUONGEZA USALAMA WA ANGA NCHINI - TCAA

soma pia


RADA MPYA KUONGEZA USALAMA WA ANGA NCHINI - TCAA

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

Mamlaka ya Usimamizi wa Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), inatarajia kufanya majaribio ya kwanza ya mfumo wa rada ya kuongozea ndege nchini unaojengwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA). 

Akizungumza na wanahabari waliofanya ziara ya kutembelea ujenzi huo, Msimamizi wa Ujenzi wa jengo lililokuwa ikifungwa rada hiyo jijini Dar es Salaam, Steven Mwakisasa amesema ujenzi wa jengo hilo umekamilika na ufungaji wa vifaa unaendelea hivyo ifikapo Desema 21 wataweza kufanya majaribio. 

"Kama mnavyoona wanahabari kila kitu kimeshafanyika tunachomalizia ni mitambo midogo midogo inayotarajia kukamilika ifikapo wiki ijayo na tufanye majaribio ili kuona ni wapi pa kurekebisha au tuongeze kitu gani?," amesema Mwakisasa.

Nae mwongoza Ndege Mkuu wa TCAA, Justine Ncheye amesema mara baada ya kukamilika na kuanza kufanya kazi, mfumo huo utaimarisha zaidi ulinzi wa anga la Tanzania. Amesema kwa kiasi kikubwa rada hiyo pamoja na zile zitakazojengwa Mwanza, Songwe na Kilimanjaro zitasimamiwa na TCAA ikiwamo kuziongoza ili kuhakikisha ulinzi unaimarishwa zaidi. 

Jiwe la msingi la ujenzi wa mfumo huo wa rada liliwekwa Aprili 2, 2018 na Rais John Magufuli na utagharimu Sh67 bilioni zikijumuisha mfumo wa rada uliojengwa katika viwanja vya ndege vya Mwanza, Kilimanjaro na Songwe.
Jengo lililofungwa rada mpya kwa ajili ya kuongozea ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam. 
Msimamizi wa Ujenzi wa jengo lililokuwa ikifungwa rada hiyo jijini Dar es Salaam, Steven Mwakisasa akitoa ufafanuzi juu ya masuala yanayohusu ujenzi huo. 
Mwongoza Ndege Mkuu wa TCAA, Justine Ncheye akieleza machache juu ya ujenzi huo wa rada mpya. 
Wanahabari waliofanya ziara katika mnara wa kuongozea ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam.



Hivyo makala RADA MPYA KUONGEZA USALAMA WA ANGA NCHINI - TCAA

yaani makala yote RADA MPYA KUONGEZA USALAMA WA ANGA NCHINI - TCAA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala RADA MPYA KUONGEZA USALAMA WA ANGA NCHINI - TCAA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/rada-mpya-kuongeza-usalama-wa-anga.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "RADA MPYA KUONGEZA USALAMA WA ANGA NCHINI - TCAA"

Post a Comment

Loading...