Loading...
title : TAKUKURU YAELEZA ILIVYOKUTA BAHASHA YA KAKI MEZANI KWA WAZIRI LUKUVI
link : TAKUKURU YAELEZA ILIVYOKUTA BAHASHA YA KAKI MEZANI KWA WAZIRI LUKUVI
TAKUKURU YAELEZA ILIVYOKUTA BAHASHA YA KAKI MEZANI KWA WAZIRI LUKUVI

KAIMU Kamishna Msaidizi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba, Maendeleo ya Makazi Wilson Luge (39) ameieleza Mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam kuwa fedha alizoenda kuhakiki katika ofisi ya Waziri wa Ardhi zinazodaiwa kutolewa kama rushwa kwa Waziri William Lukuvi zilikuwa zimehifadhiwa katika mfuko wa kaki.
Luge ameyasema hayo leo Desemba 11, 2018 wakati anajibu swali la Wakili wa utetezi Imani Madega dhidi ya kesi ya tuhuma za rushwa ya Sh. Milioni 90 kwa Waziri wa Ardhi, William Lukuvi inayomkabili Mkurugenzi wa Kampuni ya Kiluwa Steal Group Co.ltd na Kiluwa Free Processing Zone,Mohamed Kiluwa alipokuwa akitoa ushahidi wake mbele ya Hakimu Mkazi Samwel Obasi.
Amedai mahakamani hapo kuwa Julia 16 mwaka huu akiwa kazini kati ya saa saba mchana hadi saa 10 jioni, walikuwa wanaangalia mfumo wa kielekroniki wanaoutumia kama unafanya kazi vizuri, Esquires na Kamishna Mkuu wa Ardhi Mary Makondo na kuwaelekeza waende ofisi ya Waziri Lukuvi.
Pia amedai walipoingia walikuta watu mbalimbali huku mezani kukiwa na mfuko wa kaki uliokuwa umefungwa ambao hakujua ndani yake kulikuwa na nini na kwamba mfuko huo ulifunguliwa na maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru na kutoa fedha ambazo ni mabunda manne ya Dola za Marekani 40,000 ambapo waliwataka yeye na Hellen Philipo walihakiki fedha hizo.
Mapema akiongozwa kutoa ushahidi na Wakili wa Takukuru Maghela Ndimbo, shahidi huyo wa sita amedai Julai 16, mwaka huu alikuwa ofisini kwake Kanda ya Dar es Salaam ambayo zamani ilikuwa Makao Makuu ya Wizara hiyo.Alidai kati ya saa saba hadi saa 10 jioni, walikuwa wanaangalia mfumo wa kielekroniki wanaoutumia kama unafanya kazi vizuri ambapo Kamishna Mkuu wa Ardhi, Mary Makondo aliwaita akiwaelekeza waende ofisi ya Waziri Lukuvi.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>
Hivyo makala TAKUKURU YAELEZA ILIVYOKUTA BAHASHA YA KAKI MEZANI KWA WAZIRI LUKUVI
yaani makala yote TAKUKURU YAELEZA ILIVYOKUTA BAHASHA YA KAKI MEZANI KWA WAZIRI LUKUVI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TAKUKURU YAELEZA ILIVYOKUTA BAHASHA YA KAKI MEZANI KWA WAZIRI LUKUVI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/takukuru-yaeleza-ilivyokuta-bahasha-ya.html
0 Response to "TAKUKURU YAELEZA ILIVYOKUTA BAHASHA YA KAKI MEZANI KWA WAZIRI LUKUVI"
Post a Comment