Loading...
title : WWF WAANDESHA MAFUNZO YA MAWASILIANO
link : WWF WAANDESHA MAFUNZO YA MAWASILIANO
WWF WAANDESHA MAFUNZO YA MAWASILIANO
Na Yeremias Ngerangera…Bagamoyo.
Mfuko wa hifadhi ya mazingira wa dunia (WWF-World Wide Fund for Nature) unaendesha mafunzo kwa viongozi wa jumuiya za uhifadhi kuwajengea uwezo wa kuimarisha mawasiliano kati ya wanajumuiya na nje ya Jumuiya. Mafunzo hayo yanafanyika katika Hoteli ya Millenium sea breeze mjini Bagamoyo ambapo washiriki zaidi ya 48 kutoka mikoa ya lindi ,Mtwara, Pwani na Ruvuma wanashiriki mafunzo hayo ya mawasiliano thabiti kwa lengo la kujengewa uwezo wa kufanya mawasiliano na wananchi kwenye maeneo yao ya uhifadhi .
Akifungua mafunzo hayo Drt Severin Kalonga aliwataka washiriki wa mafunzo hayo kujifunza mbinu, njia na namna ya kufanya mawasiliano na jamii zilizopo katika mazingira yao ili waweze kutoa ujumbe kwa jamii ukiwa sahihi kwa watu sahihi na kwa wakati sahihi na mwishowe kupatikana kwa matokeo chanya kwa wakati. Awali Drt Kalonga aliwaeleza washiriki wa mafunzo hayo namna WWF inavyofanya kazi katika kuhakikisha hifadhi zilizopo zinaendelea kutunzwa na kubaini njia pekee ya kuendelea kutunza hifadhi hizo ni kuendelea kutoa elimu ya uhifadhi kwa wananchi kwa kuwa na mawasiliano yaliyorafiki na viongozi wao wa jumuiya.
Aidha Kalonga aliwaambia washiriki hao kuwa upangaji wa matumizi bora ya ardhi yanaumuhimu mkubwa katika jamii lakini akabainisha kuwa mbinu ,njia na namna ya kufikisha ujumbe kwa wananchi kwa viongozi wa jumuiya akazitiia mashaka. Profesa Noah Sitati naye alisema katika uhifadhi wanakumbana na changamoto nyingi sana ikiwa ni pamoja na shughuli za kibinadamu kama kilimo na ufugaji kufanyika ndani ya hifadhi hivyo kuathiri wanyamapori na ukataji hovyo wa misitu.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala WWF WAANDESHA MAFUNZO YA MAWASILIANO
yaani makala yote WWF WAANDESHA MAFUNZO YA MAWASILIANO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WWF WAANDESHA MAFUNZO YA MAWASILIANO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/wwf-waandesha-mafunzo-ya-mawasiliano.html
0 Response to "WWF WAANDESHA MAFUNZO YA MAWASILIANO"
Post a Comment