Loading...

TAMISEMI yapiga marufuku kufanya uteuzi wa nafasi za Walimu kwa rushwa

Loading...
TAMISEMI yapiga marufuku kufanya uteuzi wa nafasi za Walimu kwa rushwa - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TAMISEMI yapiga marufuku kufanya uteuzi wa nafasi za Walimu kwa rushwa, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TAMISEMI yapiga marufuku kufanya uteuzi wa nafasi za Walimu kwa rushwa
link : TAMISEMI yapiga marufuku kufanya uteuzi wa nafasi za Walimu kwa rushwa

soma pia


TAMISEMI yapiga marufuku kufanya uteuzi wa nafasi za Walimu kwa rushwa




Rais wa Chama cha Walimu Tanzania CWT Leah Ulaya akizungumza katika mkutano katika ufunguzi wa mkutano wa CWT uliohusisha Wenyeviti wa Mikoa,Wilaya na Makatibu mikoa Picha na Heri Shaban
Na HERI SHAABAN, MOROGORO

Naibu katibu Mkuu Elimu, Ofisi ya Rais TAMISEMI Tixon Nzunda akizungumza na viongozi wa Chama cha Walimu  Tanzania CWT Mkoani Morogoro Leo katika mkutano ulioshirikisha Wenyeviti wa mikoa,Wilaya pamoja na makatibu wa mikoa (Kulia)Rais wa CWT Leah Ulaya na makamu wa Rais Christopher Banda Picha na Heri Shaban
Baadhi ya Wenyeviti na Makatibu wa Mikoa na Wilaya wa Chama cha Walimu Tanzania CWT wakiwa katika mkutano wa chama hicho Mkoani Morogoro pichani wakiimba wimbo wa Mshikamano PICHA NA HERI SHAABAN

SERIKALI yapiga Marufuku kufanya nafasi za uteuzi za Walimu kwa Kitumia rushwa badala yake nafasi hizo ziteuliwe kwa kufuata uwezo na sifa za Mwalimu  katika uwajibikaji.


Tamko hilo limetolewa Mkoani Morogoro Leo na Naibu KATIBU Mkuu Elimu, Ofisi ya Rais TAMISEMI Tixon Nzuunda, katika ufunguzi wa mkutano wa cha Chama Walimu (CWT) Tanzania kilichowashirikisha, Wenyeviti wa Mikoa ,Wilaya pamoja na Makatibu wa mikoa .

"Kuanzia sasa TAMISEMI inapiga Marufuku Mchezo mchafu wa nafasi za uteuzi wa Walimu na upandishaji madaraja kwa kutumia rushwa badala yake nafasi hizi za uteuzi atateuliwa mtu kwa weledi, uhaminifu na uwezo wa kazi "alisema Nzunda

Nzunda alisema kila mwalimu atateuliwa kwa kufuata uwezo na sifa katika suala la upandishaji madaraja (promosheni)na kufuata utendaji kazi kutokana na mchango wake katika Taaluma.

Aidha alisema Walimu watoro na wanaofundisha vipindi nusu na wasiofundisha wote hawawezi kupandishwa daraja.

Aliwataka wadhibiti utoro wa Walimu shuleni  na kuongeza taaluma kwa kuweka Mpango mkakati wa malengo na kuweka heshima ili shule ziweze kupata adhi.

Pia aliwataka waimalishe mawasiliano katika vyama vya Walimu kuanzia ngazi ya Kata hadi Wilaya hadi TAIFA zikitokea changamoto wazitatue.

Wakati huohuo alisema Walimu watakaovujisha mitihani, kuuza,kuonyeha udanganyifu katika  mitihani likitokea unachishwa kazi kuanzia mratibu Elimu kata  na wengine wote waliohusika kuondolewa katika UTUMISHI wa umma  na kupelekwa mahakamani.

Alielezea uchache wa Walimu shule za Msingi alisema ajira mpya inatarajia kuanza kwa ajili ya Walimu wapya, Aliagiza Maofisa  Msingi kutoa taarifa za Walimu wanaokufa na walimu wanaostaafu pia kuacha kutembeza viboko kwa Wanafunzi shuleni sio vitendo vizuri vinadhalilisha utu wa mwalimu.


Kwa upande wake Rais wa Chama cha Walimu Tanzania CWT Leah Ulaya alisema Wanachama bado wana imani na Chama cha Walimu Tanzania CWT hivyo watumie nafasi hiyo kujadili masuala ya Walimu na changamoto zao.


Rais wa CWT Leah aliwataka watumie nafasi hiyo vizuri katika kutetea masilahi ya Walimu ikiwemo upandishwaji madaraja,awali walishafanya vikao na maofisa elimu nchi nzima na baadhi ya maofisa ELIMU wanakaimu nafasi za ukurugenzi wa Halmashauri.


Aliwataka Walimu kujitafakali upya na kuweka Mpango kazi wametoka wapi na wanaelekea Wapi.

"Tumieni  nafasi hii kuakikisha CWT inasimama imara na kutetea maslahi ya Wanachama na Walimu     kwa Jumla" alisema Leah



Hivyo makala TAMISEMI yapiga marufuku kufanya uteuzi wa nafasi za Walimu kwa rushwa

yaani makala yote TAMISEMI yapiga marufuku kufanya uteuzi wa nafasi za Walimu kwa rushwa Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TAMISEMI yapiga marufuku kufanya uteuzi wa nafasi za Walimu kwa rushwa mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/tamisemi-yapiga-marufuku-kufanya-uteuzi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "TAMISEMI yapiga marufuku kufanya uteuzi wa nafasi za Walimu kwa rushwa"

Post a Comment

Loading...