Loading...
title : TIC champongeza JPM kuionya TRA kuacha Uonevu wa Ukusanyaji na ukadiriaji viwango vya kodi wafanyabiashara na wawekezaji.
link : TIC champongeza JPM kuionya TRA kuacha Uonevu wa Ukusanyaji na ukadiriaji viwango vya kodi wafanyabiashara na wawekezaji.
TIC champongeza JPM kuionya TRA kuacha Uonevu wa Ukusanyaji na ukadiriaji viwango vya kodi wafanyabiashara na wawekezaji.
Mwambawahabari
Hussein Ndubikile
Mwamba wa Habari
Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimempongeza Rais Dkt. John Magufuli kwa kutoa tamko linaoitaka Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kutoza na kufanya ukadiriaji wa makusanyo ya kodi bila uonevu na kuiagiza kutenda haki na kufuata taratibu ili kuendelea kuwavutia na kuwatengezea mazingira rafiki wawekezaji wa ndani nje kuendelea kuwekeza nchini.
Aidha, kituo hicho kimesema tamko la onyo hilo litasaidia wawekezaji wa ndani na nje kuamini Serikali ya Awamu ya Tano haina ukandimizi kwao bali ina dhamira ya dhati kuwakaribisha kuwekeza katika sekta mbalimbali.
Pongezi hizo imekuja siku moja baada ya Rais Magufuli kuionya mamlaka hiyo akiwa kwenye ziara ya Uzinduzi wa uwekaji jiwe la msingi la Mradi wa Maji wilayani Arumeru mjini Arusha ambapo aliwaonya baadhi ya watendaji kuachakuwakadiria wafanyabiashara viwango vikubwa vya kodi hali inayowafanya wakwepe kulipa.
Pongezi hizo zimetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Geoffrey Mwambe katika Kongamano lililowakutanisha wawekezaji wa ndani na kutoka China ambapo limejadili ushirikiano wa uwekezaji na kibiashara baina ya nchi hizo.
Amesema kuwa tamko hilo litasaidia wawekezaji wengi kuchangamkia fursa za uwekezaji zililopo nchini huku na kusisitiza hata wafanyabiashara wamelipokea kwa furaha kwani litawaondolea adha na kuwakatisha tama ya kufunga biashara zao.
“ Tunafurahi na tumelipokea tamko la Rais Magufuli kwa TRA litatengeneza mahausiano mema kati ya wafanyabiashara, wawekezaji na Serikali itafungua fursa za uwekezaji nchini,” amesema.
Amebainisha kuwa tamko la kuitaka TRA kuweka utaratibu mzuri wa wawekezaji na wafanyabiashara kufanya malipo ya kodi utasaidia kuliongeza taifa mapato yatakayochangia maendeleo ya nchi.
Amefafanua kuwa China ni nchi inayoongoza kwa miradi ya uwekezaji nchini ambapo ipo takribani 723 ambayo imeachangia ajira 84,000 na kwamba TIC itaendelea kushirikiana na wawekezaji kutoka nchi hiyo.
Kwa upande wake, Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji, Joseph Kakunda amesema ni muhimu kuwakaribisha wawekezaji hao kuwekeza kwenye viwanda vya mazao kwani kutasaidia kuyapandisha hadhi mazao yetu na kuuza nje,
Waziri Kakunda amesema uwekezaji wa viwanda hivyo utapunguza uagizaji wa bidhaa nje na kulipatia taifa fedha za kigeni na kwamba nchi hiyo ina mtaji wa uwekezaji wa Sh bilioni 5.8 za Kimarekani.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini (tpsf), Godfrey Simbeye amebainisha kuwa taasisi itaendelea kushirikiana na wawekezaji wa ndani na nje ili kuhakikisha ifikapo mwaka 2025 nchi inafikia uchumi wa kati kupitia uchumi wa viwanda.
Katika hatua nyingine amempongeza Rais Magufuli kwa kuikemea TRA na kusisitiza onyo hilo litapunguza unyayasaji na kwamba tayari taasisi hiyo imeanzisha dawati la kuwasiliana na wawekezaji kutoka China.
Balozi wa China nchini, Wang Ke amesema kongamano hilo litasaidia kutengeneza mazingira rafiki kwa wawekezaji wa China kuja kuwekeza huku akikazia tayari nchi imeshariki katika miradi mbalimbali ikiwemo ya ujenzi wa Uwanja wa Taifa, Maabara ya Kisasa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.
Mwenyekiti wa Baraza la Uwezeshaji, Uendelezaji Ushirikiano wa Nchi za Kusini na Kusisni, Lyu Xinhua amesema kutokana mazingira ya uwekezaji kuwa mazuri anaamini waekezaji wengi watachangmkia fursa za uwekezaji.
Hivyo makala TIC champongeza JPM kuionya TRA kuacha Uonevu wa Ukusanyaji na ukadiriaji viwango vya kodi wafanyabiashara na wawekezaji.
yaani makala yote TIC champongeza JPM kuionya TRA kuacha Uonevu wa Ukusanyaji na ukadiriaji viwango vya kodi wafanyabiashara na wawekezaji. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TIC champongeza JPM kuionya TRA kuacha Uonevu wa Ukusanyaji na ukadiriaji viwango vya kodi wafanyabiashara na wawekezaji. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/tic-champongeza-jpm-kuionya-tra-kuacha.html
0 Response to "TIC champongeza JPM kuionya TRA kuacha Uonevu wa Ukusanyaji na ukadiriaji viwango vya kodi wafanyabiashara na wawekezaji."
Post a Comment