Loading...
title : TFDA YAFUNGUA MAFUNZO YA WACHUNGUZI WA MAABARA ZA DAWA KWA BARA LA AFRIKA
link : TFDA YAFUNGUA MAFUNZO YA WACHUNGUZI WA MAABARA ZA DAWA KWA BARA LA AFRIKA
TFDA YAFUNGUA MAFUNZO YA WACHUNGUZI WA MAABARA ZA DAWA KWA BARA LA AFRIKA
NaEmmanuel Masaka,Globu ya jamii
MAMLAKA ya Chakula na Dawa nchini Tanzania(TFDA) imefungua mafunzo ya wachunguzi wa maabara za dawa kwa nchi za Afrika jijini Dar es salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam katika Mkutano wa Kanda kwa nchi za Afrika, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Dk.Faustine Ndugulile ameeleza kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wachunguzi wa Maabara .
Dk.Ndugulile ameeleza kwa sasa duniani kumekuepo na usugu mkubwa kwenye baadhi ya vyakula ambavo haviivi vizuri au walaji wa nyama na mayai kutochunguza kwa makini kama kuna asilimia yoyote ambayo italeta madhara Kwenye miili yao pindi watakapokula vyakula ambavo si salama kwa afya zao.
Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya dawa na chakula ( TFDA)Adam Fimbo amefafanua zaidi kuwa lengo la mafunzo hayo si tu kuwajengea uwezo wachunguzi wa maabara bali pia kutoa elimu kwa jamii jinsi gani wanatakiwa kuepuka vyakula ambavo vitaleta madhara baadae katika miili yao.
Fimbo amesema washiriki wa mafunzo hayo wapo 30 na nchi ambazo zinazoshiriki ni 22.Baadhi ya nchi hizo ni Algeria, Angola, Benin, Botswana, Burkina Faso, Burundi, Chad, DRC, Egypt, Kenya,Madagascar, Malawi, Mali, Mauritania, Morocco, Nigeria, SieraLeone, South Africa, Sudan, Uganda, Tanzania na Zimbabwe.
Pia amewasisitiza washiriki kuzingatia mafunzo hayo kwa ajili ya kunusuru na kupunguza kabisa uwezekano wa baadhi ya magonjwa ambayo si ya lazima endapo tutaweza kuyapatia ufumbuzi mapema .
Naibu waziri wa Afya maendeleo Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Dk.Faustine Ndugulile akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo wachunguzi wa maabara za dawa kwa nchi za Africa, leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa TFDA,Adam fimbo akizungumza na waandishi wa habari (hawapi pichani) leo jijini Dar es Salaam katika mafunzo ya kuwajengea uwezo wachunguzi wa maabara za dawa kwa nchi za africa.
Makamu Mkurugenzi wa Maabara kutoka Nigeria Dkt.Flosade Oluwabamieo akifafanua jambo mbele washiliki wa mafunzo ya wachunguzi wa maabara za dawa leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya washiriki wakimzikiliza Naibu Waziri wa Afya Maendeo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dr. Faustine Ndungulile (hayupo pichani) alipokua akifungua mafunzo ya wachunguzi wa maabara za dawa kwa nchi za Africa, leo jijini Dar es Salaam.(picha na Emmanuel Massaka wa MMG)
Hivyo makala TFDA YAFUNGUA MAFUNZO YA WACHUNGUZI WA MAABARA ZA DAWA KWA BARA LA AFRIKA
yaani makala yote TFDA YAFUNGUA MAFUNZO YA WACHUNGUZI WA MAABARA ZA DAWA KWA BARA LA AFRIKA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TFDA YAFUNGUA MAFUNZO YA WACHUNGUZI WA MAABARA ZA DAWA KWA BARA LA AFRIKA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/tfda-yafungua-mafunzo-ya-wachunguzi-wa.html
0 Response to "TFDA YAFUNGUA MAFUNZO YA WACHUNGUZI WA MAABARA ZA DAWA KWA BARA LA AFRIKA"
Post a Comment