Loading...

UPATIKANAJI WA NAKALA ZA HUKUMU NA NYARAKA NYINGINE ZA MAHAKAMA WABORESHWA ZAIDI

Loading...
UPATIKANAJI WA NAKALA ZA HUKUMU NA NYARAKA NYINGINE ZA MAHAKAMA WABORESHWA ZAIDI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa UPATIKANAJI WA NAKALA ZA HUKUMU NA NYARAKA NYINGINE ZA MAHAKAMA WABORESHWA ZAIDI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : UPATIKANAJI WA NAKALA ZA HUKUMU NA NYARAKA NYINGINE ZA MAHAKAMA WABORESHWA ZAIDI
link : UPATIKANAJI WA NAKALA ZA HUKUMU NA NYARAKA NYINGINE ZA MAHAKAMA WABORESHWA ZAIDI

soma pia


UPATIKANAJI WA NAKALA ZA HUKUMU NA NYARAKA NYINGINE ZA MAHAKAMA WABORESHWA ZAIDI

Na Mary Gwera, Mahakama ya Tanzania
Mahakama ya Tanzania iliingia mkataba na Shirika la Posta kuhakikisha kuwa huduma ya kusambaza nyaraka mbalimbali za Mahakama inatolewa kwa nchi nzima. Mkataba huu chini ya huduma mpya ya Posta mlangoni (The post at your door step) iliyoanzishwa na Shirika la Posta, umelipa jukumu la kukusanya na kusafirisha/kusambaza nakala za hukumu na nyaraka mbalimbali za Mahakama na kuzifikisha kwa wahusika kulingana na anuani zao na mahali walipo (Anuani za makazi).

Kwa kipindi kirefu kumekuwa na malalamiko miongoni mwa wananchi/wateja wa Mahakama juu ya usumbufu katika upatikanaji wa Nakala za hukumu na baadhi ya nyaraka za Mahakama, hali ambayo kwa namna moja au nyingine ilisababishwa kwa kutokuwa na taarifa sahihi za Mdaawa/Mteja na utaratibu stahiki wa ufikishaji wa nyaraka hizo. Mahakama ya Tanzania katika utekelezaji wake wa majukumu mbalimbali inawalenga wateja wake ili kuhakikisha haki inatolewa kwa wakati na kuimarisha imani ya Wadau kwa Mahakama. Utoaji wa huduma kwa wateja pamoja na mambo mengine unajumuisha utoaji wa nyaraka mbalimbali kama nakala za hukumu, wito wa kuitwa Mahakamani (Sumons).

Aidha; nyaraka muhimu zinazosambazwa kupitia huduma ya Posta Mlangoni ni Nakala za Hukumu ‘Judgment’, ‘Summons’ wito wa Mahakama, Mwenendo wa shauri/mashauri ‘Proceedings’, Maamuzi ‘Rulings’,  Amri ‘Order’, Tuzo ‘Award’/ ‘Decree’. Akizungumza kabla ya utiani saini wa mkataba huo Aprili, 2018, Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Bw. Hussein Kattanga alisema kuwa hatua hii ni mwendelezo wa maboresho mbalimbali yanayoendelea kufanyika ili kuwafikia wananchi kwa karibu zaidi.
 Mtendaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga (katikati) akitia saini Mkataba wa utoaji huduma ya Posta mlangoni (The post at your door step), anayeshuhudia kulia ni Msajili Mkuu- Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati aliyeketi kushoto ni Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Bw. Hassan Mwang’ombe, wanaoshuhudia (waliosimama) ni baadhi ya Viongozi/Maafisa kutoka Mahakama na Shirika la Posta.
Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Bw. Hassan Mwang’ombe akitia saini Mkataba huo.
Makabidhiano ya Mikataba hiyo mara baada ya kuhitimisha zoezi la utiaji saini. Kulia ni Mtendaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga na kushoto ni Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Bw. Hassan Mwang’ombe.
 Msajili Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati (kulia) akiongea jambo mara baada ya utiaji saini wa Mkataba huo.
(Picha na Mary Gwera, Mahakama)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala UPATIKANAJI WA NAKALA ZA HUKUMU NA NYARAKA NYINGINE ZA MAHAKAMA WABORESHWA ZAIDI

yaani makala yote UPATIKANAJI WA NAKALA ZA HUKUMU NA NYARAKA NYINGINE ZA MAHAKAMA WABORESHWA ZAIDI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala UPATIKANAJI WA NAKALA ZA HUKUMU NA NYARAKA NYINGINE ZA MAHAKAMA WABORESHWA ZAIDI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/upatikanaji-wa-nakala-za-hukumu-na.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "UPATIKANAJI WA NAKALA ZA HUKUMU NA NYARAKA NYINGINE ZA MAHAKAMA WABORESHWA ZAIDI"

Post a Comment

Loading...