Loading...
title : WANAOIHUJUMU ATCL SASA KUFUATILIWA KWA KARIBU.
link : WANAOIHUJUMU ATCL SASA KUFUATILIWA KWA KARIBU.
WANAOIHUJUMU ATCL SASA KUFUATILIWA KWA KARIBU.
Na John Nditi, Morogoro
NAIBU waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi, Atashasta Nditiye ameiagiza Baraza la Wafanyakazi la Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) pamoja na Menejimenti ya Kampuni kuimarisha kitengo cha masoko na kufanya ufuatiliaji kwa watumishi na mawakala wanaoihujumu Kampuni hiyo.
Naibu Waziri alisema hayo katika hotuba yake ya ufunguzi wa kikao cha tatu cha baraza la wafanyakazi wa ATCL lililofanyika mjini Morogoro.
Alisema , kwa muda mrefu kumekuwa na manenoo mengi yanayosemwa juu ya kuwepo hujuma dhidi ya Ndege za ATCL hasa kwenye njia ya Kilimanjaro na Mbeya .Mbali na njia hizo pia huduma hizo zinafanywa kwa maeneo mengine ambapo wateja wanapohitaji huduma za ATCL huambiwa kuwa ndege zimejaa wakati jambo hilo si kweli na matokeo yake ndege zinaondoka bila kujaa abiria.
“ Baadhi ya makawala wanaouza tiketi za ATCL wanaonwa na makampuni mengine ya Ndege ili wajaze kwanza ndege zao kwa kutoa maelezo kwa wateja wanaohitaji kusafiri na ndege zetu za umma kuwa zimejaa , lakini baadaye zinaondoka bila kujaa abiria” alisema Naibu Waziri Nditiye.
Naibu Waziri huyo alisema “ Huduma za ndege zetu ni nzuri na nauli yake ni ndogo na pia ndege zetu zote ni mpya lakini hazijai tofauti na za makampuni binafsi ambayo bei zake ni za juu na huduma zao hazifanani na za ATCL “ alisema Naibu Waziri Nditiye .
Naibu waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi, Atashasta Nditiye ( kushoto) akijadiliana jambo na Mkurugenzi mkuu wa ATCL, Ladislaus Matindi ( wa pili kushoto ) baada ya Naibu Waziri kufungua kikao cha tatu cha baraza la wafanyakazi wa ATCL lililofanyika mjini Morogoro.
Naibu waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano , Mhandisi Atashasta Nditiye ( kulia ) akijadiliana jambo na Mkurugenzi mkuu wa ATCL, Ladislaus Matindi ( kushoto ) kwa ajili ya kufungua kikao cha tatu cha baraza la wafanyakazi wa ATCL kilichofanyika mjini Morogoro.
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa ATCL wakimsilikiza Naibu waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi, Atashasta Nditiye ( hayupo pichani ) alipofungua kikao cha tatu cha baraza hilo mjini Morogoro.
Hivyo makala WANAOIHUJUMU ATCL SASA KUFUATILIWA KWA KARIBU.
yaani makala yote WANAOIHUJUMU ATCL SASA KUFUATILIWA KWA KARIBU. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WANAOIHUJUMU ATCL SASA KUFUATILIWA KWA KARIBU. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/wanaoihujumu-atcl-sasa-kufuatiliwa-kwa.html
0 Response to "WANAOIHUJUMU ATCL SASA KUFUATILIWA KWA KARIBU."
Post a Comment