Loading...
title : WAZIRI HASUNGA AMUAGIZA KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO KUMSIMAMISHA KAZI MTUMISHI MMOJA KWENYE TIMU YA OPARESHINI KOROSHO
link : WAZIRI HASUNGA AMUAGIZA KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO KUMSIMAMISHA KAZI MTUMISHI MMOJA KWENYE TIMU YA OPARESHINI KOROSHO
WAZIRI HASUNGA AMUAGIZA KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO KUMSIMAMISHA KAZI MTUMISHI MMOJA KWENYE TIMU YA OPARESHINI KOROSHO
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Mtwara
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe kumsimamisha kazi mtumishi George Mboje na kumuondoa kwenye timu ya Operesheni Korosho.
Pamoja na kumundoa kwenye timu hiyo pia Katibu Mkuu ametakiwa kumuondoa kwenye Bodi ya Nafaka na Mazao mchanganyiko."Katibu Mkuu, nataka umuondoe huyu George kwenye hii timu na pia sitaki kumuona kwenye Bodi na Taasisi yoyote katika Wizara ya Kilimo" Alisisitiza Mhe Hasunga .
Mhe Hasunga ametoa agizo hilo leo tarehe 4 Disemba 2018 wakati akizungumza kwenye kikao kazi cha Watendaji wa timu ya Oparesheni korosho kilichofanyika katika ukumbi wa CBT Mkoani Lindi na wakati wa kikao kazi na watendaji wa serikali sambamba na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Mkoani Lindi katika ziara yake ya kikazi aliyoianza leo tarehe 4 Disemba 2018.
George Mboja ambaye yupo kwenye timu ya Oparesheni Korosho akiwakilisha Bodi ya Nafaka na Mazao mchanganyiko anatuhumiwa kwa Utovu wa nidhamu sambamba na kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo wakati wa Oparesheni Korosho inayoendelea nchini.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye kikao kazi na watendaji wa serikali sambamba na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Mkoani Lindi katika ziara yake ya kikazi aliyoianza leo tarehe 4 Disemba 2018 mkoani humo. (Picha Na Mathias Canal-Wizara ya Kilimo).
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye kikao kazi na watendaji wa serikali sambamba na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Mkoani Lindi katika ziara yake ya kikazi aliyoianza leo tarehe 4 Disemba 2018 mkoani humo.
Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mhe Sarah Chiwamba, Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mhe Rukia Muwango na Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mhe Christopher Ngubiagai wakisikiliza kwa makini hotuba ya Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati akizungumza kwenye kikao kazi na watendaji wa serikali sambamba na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Mkoani Lindi katika ziara yake ya kikazi aliyoianza leo tarehe 4 Disemba 2018 mkoani humo.
Hivyo makala WAZIRI HASUNGA AMUAGIZA KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO KUMSIMAMISHA KAZI MTUMISHI MMOJA KWENYE TIMU YA OPARESHINI KOROSHO
yaani makala yote WAZIRI HASUNGA AMUAGIZA KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO KUMSIMAMISHA KAZI MTUMISHI MMOJA KWENYE TIMU YA OPARESHINI KOROSHO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI HASUNGA AMUAGIZA KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO KUMSIMAMISHA KAZI MTUMISHI MMOJA KWENYE TIMU YA OPARESHINI KOROSHO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/waziri-hasunga-amuagiza-katibu-mkuu.html
0 Response to "WAZIRI HASUNGA AMUAGIZA KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO KUMSIMAMISHA KAZI MTUMISHI MMOJA KWENYE TIMU YA OPARESHINI KOROSHO"
Post a Comment