Loading...
title : WAZIRI WA MADINI AELEZEA MCHANGO WA SEKTA YA MADINI KATIKA KUFIKIA UCHUMI WA KATI , TIC YAZUNGUMZIA MABORESHO YA SERA NA SHERIA
link : WAZIRI WA MADINI AELEZEA MCHANGO WA SEKTA YA MADINI KATIKA KUFIKIA UCHUMI WA KATI , TIC YAZUNGUMZIA MABORESHO YA SERA NA SHERIA
WAZIRI WA MADINI AELEZEA MCHANGO WA SEKTA YA MADINI KATIKA KUFIKIA UCHUMI WA KATI , TIC YAZUNGUMZIA MABORESHO YA SERA NA SHERIA
WAZIRI wa Madini Angela Kairuki amesema ili kufikia malengo ya mpango wa taifa wa maendeleo ambao unaelekeza kuwa ifikapo mwaka 2025 Tanzania iwe imefikia uchumi wa kati, sekta ya madini inalazimika kuongeza mchango katika pato la taifa kutoka asilimia 4.8 ya sasa kufikia asilimia 10 mwaka 2025.
Ametoa kauli hiyo wakati wa ufunguzi wa kongamano la uwekezaji katika sekta ya madini kati ya Tanzania na China lililofanyika jijini Beijing nchini China.
"Ili kufikia malengo ya mpango wa taifa wa maendeleo ambao unaelekeza kuwa ifikapo mwaka 2025 Tanzania iwe imefikia uchumi wa kati, sekta ya madini inalazimika kuongeza mchango katika pato la taifa kutoka asilimia 4.8 ya sasa kufikia asilimia 10 mwaka 2025," amefafania Waziri Kairuki.
Wakati Waziri Kairuki anazungumza washiriki wa Kongamono la siku moja la uwekezaji katika sekta ya madini kati ya Tanzania na China walikuwa wakisikiliza kwa makini fursa zilizopo nchini Tanzania.Pia mada mmbalimbali zilizowasilishwa katika kongamo hilo ambalo limelenga kuhamasisha ubia katika sekta ya madini ikiwemo kuvutia mitaji zaidi, teknolojia mpya kwenye utafiti, uchimbaji na uchakataji wa madini ili kuyaongezea thamani.
Akifungua Kongamano hilo la kwanza la aina yake kuandaliwa na Wizara ya madini kwa ushirikiano na kituo cha uwekezaji Tanzania na ubalozi wa Tanzania nchini China, Waziri wa Madini Angela Kairuki, ametumia jukwa hilo kuelezea mipango ya wizara yake katika kukuza sekta ya madini nchini.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha uwekezaji Tanzania(TIC) Geofrey Mwambe amesema nia ya Serikali katika maboresho ya sera na sheria ni kuhakikisha kuwa rasilimali za Tanzania zinawanufaisha watanzania pamoja wawekezaji.
WAZIRI wa Madini Angela Kairuki akizungumza mbele ya wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa kongamano la uwekezaji katika sekta ya madini kati ya Tanzania na China lililofanyika jijini Beijing nchini China hivi karibuni.
WAZIRI wa Madini Angela Kairuki akizungumza mbele ya Wanahabari (hawapo pichani) kuhusu ufunguzi wa kongamano la uwekezaji katika sekta ya madini kati ya Tanzania na China lililofanyika jijini Beijing nchini China hivi karibuni.
Hivyo makala WAZIRI WA MADINI AELEZEA MCHANGO WA SEKTA YA MADINI KATIKA KUFIKIA UCHUMI WA KATI , TIC YAZUNGUMZIA MABORESHO YA SERA NA SHERIA
yaani makala yote WAZIRI WA MADINI AELEZEA MCHANGO WA SEKTA YA MADINI KATIKA KUFIKIA UCHUMI WA KATI , TIC YAZUNGUMZIA MABORESHO YA SERA NA SHERIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI WA MADINI AELEZEA MCHANGO WA SEKTA YA MADINI KATIKA KUFIKIA UCHUMI WA KATI , TIC YAZUNGUMZIA MABORESHO YA SERA NA SHERIA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/waziri-wa-madini-aelezea-mchango-wa.html
0 Response to "WAZIRI WA MADINI AELEZEA MCHANGO WA SEKTA YA MADINI KATIKA KUFIKIA UCHUMI WA KATI , TIC YAZUNGUMZIA MABORESHO YA SERA NA SHERIA"
Post a Comment