Loading...
title : UJENZI BARABARA BARIADI HADI MASWA MKOANI SIMIYU WASHIKA KASI
link : UJENZI BARABARA BARIADI HADI MASWA MKOANI SIMIYU WASHIKA KASI
UJENZI BARABARA BARIADI HADI MASWA MKOANI SIMIYU WASHIKA KASI
Na Benny Mwaipaja, WFM, Simiyu
UJENZI wa barabara yenye urefu wa kilometa 50 kati ya mji wa Bariadi na Maswa mkoani Simiyu kwa kiwango cha lami, inayojengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 88, unaendelea kwa kasi ambapo hivi sasa umefikia asilimia 34.
Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini-TANROADS, mkoa wa Simiyu, Mhandisi Mohamedi Athumani, ameiambia timu ya maafisa wa Serikali inayoongozwa na Wizara ya Fedha na Mipango, inayofuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo mkoani humo kwamba mradi huo utakapo kamilika mwezi Oktoba mwakani, utafungua fursa za kibiashara na kiuchumi kwenye mkoa huo na mikoa jirani ya Mwanza, Shinyanga, Singida na nchi jirani ya Kenya.
Amesema kuwa kazi zilizofanywa na mkandarasi anayejenga barabara hiyo, Kampuni ya CHICO ya China, ni kuanza kwa ujenzi wa madaraja makubwa mawili ya Simiyu na Banhya na uinuaji wa tuta la barabara maeneo mbalimbli ya mradi.
“Kuna madaraja mengine madogo madogo (Pipe culverts 57) pamoja na makalvati madogo (Box culverts 12), kwenye kipande hiki cha Barabara chenye urefu wa kilometa 50 na mkandarasi, Kampuni ya CHICO inafanyakazi vizuri na tuna imani kwamba ujenzi wa barabara hii utakamilika ifikapo mwezi Oktoba, 2019 kama mkataba unavyoonesha” alifafanua Mhandisi Athumani.

Maafisa wa Serikali kutoka Wizara ya Maji, Wizara ya Ujenzi, miundombinu na Mawasiliano, wakiongozwa na Wizara ya Fedha na Mipango, wakipata maelezo ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami ya Bariadi hadi Maswa, (km50) wakati wa ziara ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Simiyu, ili kujua mafanikio, changamoto na mikakati ya kukabiliana na changamoto hizo.
Mchumi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Jordan Matonya, akitaka kupata ufafanuzi kuhusu utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Bariadi hadi Maswa, mkoani Simiyu, yenye urefu wa km 50, kutoka kwa Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara mkoani humo, Mhandisi Mohamedi Athumani (Hayuko pichani).
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>
Hivyo makala UJENZI BARABARA BARIADI HADI MASWA MKOANI SIMIYU WASHIKA KASI
yaani makala yote UJENZI BARABARA BARIADI HADI MASWA MKOANI SIMIYU WASHIKA KASI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala UJENZI BARABARA BARIADI HADI MASWA MKOANI SIMIYU WASHIKA KASI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/ujenzi-barabara-bariadi-hadi-maswa_13.html
0 Response to "UJENZI BARABARA BARIADI HADI MASWA MKOANI SIMIYU WASHIKA KASI"
Post a Comment