Loading...
title : WODI YA SEWA HAJI, MWANZILISHI WAKE HUYU HAPA
link : WODI YA SEWA HAJI, MWANZILISHI WAKE HUYU HAPA
WODI YA SEWA HAJI, MWANZILISHI WAKE HUYU HAPA

Sewa Haji Paroo raia wa India, alizaliwa mwaka 1851 na kufariki 1891 huko visiwani Zanzibar na kuacha historia kubwa katika maeneo ya Zanzibar na Bagamoyo kwa msaada aliokuwa anautoa kwa jamii hizo hasa kwa kujenga huduma za jamii kama shule, hospitali na visima.
Sewa Haji alikuja Tanzania mnamo mwaka 1851 huko Bagamoyo na mwaka 1897 aliweka makazi yake Zanzibar ambapo alifanya biashara na kuwa mmoja ya wafanyabiashara wakubwa visiwani humo.
Sewa Haji paroo ndiye mwanzilishi na ndiye aliyedhamini ujenzi wa hospitali ya Sewa Haji kama ilivyojulikana kwa kipindi hicho na kwa sasa inajulikana kama hospitali ya taifa Muhimbili jijini Dar es saalam, hospitali hiyo ilikuwa ikitoa huduma kwa wananchi wa kipato cha chini bure kabisa na kwa sasa Sewa Haji ni moja moja kati ya wodi maarufu katika hospitali ya taifa Muhimbili.
Pia Sewa Haji Paroo alidhamini miradi mingi zikiwemo shule, misikiti na miradi ya mingi ya kijamii huko Bagamoyo na alikuwa rafiki mzuri wa wakristo na kutoa misaada.
Hospitali ya taifa Muhimbili ilianza miaka ya 1910 hadi 1920 ikijulikana kama Sewa Haji na kufikia mwaka 1956 iliitwa hospitali ya Princess Magreth na baada ya uhuru 1961 ilijulikana kama Muhimbili hospitali na baadaye kuitwa Muhimbili medical centre mnamo mwaka 1976 na baadaye kuitwa Hospitali ya taifa Muhimbili.
Hivyo makala WODI YA SEWA HAJI, MWANZILISHI WAKE HUYU HAPA
yaani makala yote WODI YA SEWA HAJI, MWANZILISHI WAKE HUYU HAPA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WODI YA SEWA HAJI, MWANZILISHI WAKE HUYU HAPA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/wodi-ya-sewa-haji-mwanzilishi-wake-huyu.html
0 Response to "WODI YA SEWA HAJI, MWANZILISHI WAKE HUYU HAPA"
Post a Comment