Loading...
title : Yapi Merkezi yafanya usafi Ufukwe wa Coco
link : Yapi Merkezi yafanya usafi Ufukwe wa Coco
Yapi Merkezi yafanya usafi Ufukwe wa Coco
Na Chalila Kibuda ,Globu ya Jamii .
Kampuni ya Yapi Merkezi inayojenga Reli ya Kisasa imefanya usafi katika ufukwe wa Coco, ikiwa ni utunzaji wa Mazingira katika jamii inayowazunguka katika mradi wa Reli hiyo.
Akizungumza na waandishi wa Habari jioni ya leo, Mratibu wa Mazingira wa Kampuni hiyo Evodiaglory Mrengo amesema kuwa katika Ujenzi wa Reli wanatambua umuhimu wa utunzaji wa Mazingira katika kujenga afya salama kwa jamii wanayoizunguka katika miradi.
Amesema kuwa kufanya usafi Ufukwe wa Coco ni mojawapo ya kazi za kijamii na Mazingira,na kwama kila Kampuni ikipata muda wa kufanya kazi ya kijamii ni vyema ikafavya hivyo.Mrengo amesema kuwa kufanya usafi ni kuhamasisha Wafanyakazi na jamii ya Mkoa wa Dar es Salaam kuwa mstari wa mbele katika utunzaji na uhifadhi wa fukwe za bahari ikiwa ni sehemu muhimu za mapumuziko.
Mjumbe wa Serikali ya Mtaa na Mwenyekiti wa Kamati ya Mazingira Oysterbay Peter Mushi amesema wanatambua mchango wa Kampuni ya Yapi Merkezi kufanya usafi katika ufukwe wa Coco.
Kiongozi Mkuu wa Afya na Mazingira wa Kampuni ya Yapi Markezi Erdem Yuksel akizungumza kuhusiana na Kampuni hiyo kutoa mchango katika maeneo mbalimbali ikiwemo kufanya usafi katika ufukwe wa Coco leo jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Oysterbay na Mwenyekiti wa Kamati ya Mazingira wa Mtaa huo Peter Mushi akizungumza kuhusiana na Ujio wa Kampuni ya Yapi Markezi kufanya usafi katika ufukwe wa Coco,jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Mazingira wa Kampuni ya Yapi Markezi Evodiaglory Mrengo akizungumza na waandishi habari kuhusiana na usafi wa Kampuni hiyo waliofanya katika Ufukwe wa Coco ,jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Ujenzi wa Reli ya Kisasa Yapi Markezi wakifanya usafi katika ufukwe wa Coco ikiwa ni kutoa msaada kwa jamii
Hivyo makala Yapi Merkezi yafanya usafi Ufukwe wa Coco
yaani makala yote Yapi Merkezi yafanya usafi Ufukwe wa Coco Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Yapi Merkezi yafanya usafi Ufukwe wa Coco mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/yapi-merkezi-yafanya-usafi-ufukwe-wa.html
0 Response to "Yapi Merkezi yafanya usafi Ufukwe wa Coco"
Post a Comment