Loading...

Zitto Kabwe 'Kujisalimisha' TAKUKURU Kesho Ijumaa

Loading...
Zitto Kabwe 'Kujisalimisha' TAKUKURU Kesho Ijumaa - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Zitto Kabwe 'Kujisalimisha' TAKUKURU Kesho Ijumaa, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Zitto Kabwe 'Kujisalimisha' TAKUKURU Kesho Ijumaa
link : Zitto Kabwe 'Kujisalimisha' TAKUKURU Kesho Ijumaa

soma pia


Zitto Kabwe 'Kujisalimisha' TAKUKURU Kesho Ijumaa

 
 Image result for picha za zitto kabwe
 
Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, kesho anatarajia kuitikia wito wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kuhusiana na mambo aliyoandika kwenye mitandao ya kijamii.

Takukuru kupitia Naibu Mkurugenzi Mkuu wake, Brigedia Jenerali John Mbungo, ilimtaka kiongozi huyo kufika ofisini kwake kutoa ushahidi wa tuhuma alizozitoa kuwa kuna kampuni tatu za chuma zimewahonga baadhi ya viongozi wa serikali.

Sehemu ya taarifa ya wito huo ilieleza kuwa: “Tunatoa taarifa hii kupitia vyombo vya habari kumwomba Zitto Kabwe afike ofisi za Takukuru Dar es Salaam mapema iwezekanavyo ili tushirikiane katika kulishughulikia suala hili muhimu kwa mustakabali wa maendeleo ya taifa letu.”

Alipotafutwa Afisa Habari wa ACT-Wazalendo, Abdallah Khamis, kueleza ni lini kiongozi huyo atakwenda kuripoti Takukuru, alisema Zitto ataripoti Takukuru Ijumaa (kesho).

Kwenye mitandao ya kijamii Zitto alidaiwa kuandika kuwa amepata habari za kushtusha kuwa kampuni tatu za China, Russia na Uturuki zimewahonga baadhi ya watendaji wa serikali kuchelewesha mradi wa Mchuchuma na Liganga. Lengo ni kuhakikisha nchi hizo zinapata soko la chuma chao.

Aliendelea kuandika kuwa kuhujumu mradi wa Mchuchuma na Liganga ni uhaini. Baadhi hawawezi kusahau hujuma hiyo na yeyote anayeshiriki atasakwa mpaka kaburini kwake, ikibidi kuondoa kinga za watu ili liwe fundisho kwa uhujumu huu uchumi na uhai wa taifa letu.

Aliandika zaidi kuwa msamaha wa kodi kwa bomba la mafuta kutoka Uganda ni mkubwa na hauna faida kulinganisha na mradi wa Mchuchuma na Liganga utakaotoa ajira za kudumu 35,000 kuingiza fedha za kigeni bilioni 4.6 kwa mwaka na kuifanya nchi yetu kuwa na viwanda vikubwa.


Hivyo makala Zitto Kabwe 'Kujisalimisha' TAKUKURU Kesho Ijumaa

yaani makala yote Zitto Kabwe 'Kujisalimisha' TAKUKURU Kesho Ijumaa Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Zitto Kabwe 'Kujisalimisha' TAKUKURU Kesho Ijumaa mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/zitto-kabwe-kujisalimisha-takukuru.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Zitto Kabwe 'Kujisalimisha' TAKUKURU Kesho Ijumaa"

Post a Comment

Loading...