Loading...

MAFUNDI SIMU SASA KUSAJILIWA TCRA

Loading...
MAFUNDI SIMU SASA KUSAJILIWA TCRA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MAFUNDI SIMU SASA KUSAJILIWA TCRA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MAFUNDI SIMU SASA KUSAJILIWA TCRA
link : MAFUNDI SIMU SASA KUSAJILIWA TCRA

soma pia


MAFUNDI SIMU SASA KUSAJILIWA TCRA

 
 
 
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imeiagiza Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) kusajili mafundi wanaotoa huduma za matengenezo ya simu za mkononi kwa mujibu wa sheria zilizopo na kuhakikisha huduma wanaozotoa kwa wananchi zina viwango stahiki.

Agizo hilo limetolewa na Naibu Katibu Mkuu Wizara hiyo Sekta ya Mawasiliano Dk Jim Yonaz jana Jumatano Disemba 5, alipokuwa akiwatunuku vyeti vya kuhitimu mafunzo ya miezi mitano kwa mafundi simu 68 yaliyotolewa katika Chuo cha Sayansi na Teknolojia (DIT).

Dk Yonaz amewataka mafundi simu hao kutumia elimu waliyoipata katika mafunzo hayo wakaitumie kwa kuwahudumia wananchi kwa uadilifu mkubwa na kuwa mfano kwa mafundi wa aina hiyo hapa nchini.

“Kuanzisha mafunzo haya ya kurasimisha ufundi wa simu za mkononi kutawasaidia mafundi kufanya kazi kwa weledi na ufahamu lakini pia itaisaidia TCRA kutoa leseni kwa mafundi ambao kiwango chao kinafahamika.

“Yamekuja kwa wakati muafaka na naomba yaendelee kusimamiwa vyema ili mafundi simu za mikononi nchini kote waweze kupata elimu hii, ” amesema Dk Yonaz.

Aidha Dk Yonaz ametoa rai kwa wadau wa Mawasiliano nchini kubuni mipango endelevu ya kushirikiana kuchangia katika kufanikisha mafunzo hayo.


Hivyo makala MAFUNDI SIMU SASA KUSAJILIWA TCRA

yaani makala yote MAFUNDI SIMU SASA KUSAJILIWA TCRA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MAFUNDI SIMU SASA KUSAJILIWA TCRA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/mafundi-simu-sasa-kusajiliwa-tcra.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MAFUNDI SIMU SASA KUSAJILIWA TCRA"

Post a Comment

Loading...