Loading...
title : Afisa msaidiazi wa TRA kizimbani kwa kumili mali zisizolingana na kipato chake
link : Afisa msaidiazi wa TRA kizimbani kwa kumili mali zisizolingana na kipato chake
Afisa msaidiazi wa TRA kizimbani kwa kumili mali zisizolingana na kipato chake
Na Karama Kenyunko Globu ya Jamii
Aliyekuwa Afisa Msaidizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, (TRA) Godfrey Mapuga amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za kumiliki mali ya zaidi ya Sh. Milioni 720. isiyolingana na kipato chake cha sasa wala cha zamani.
Akisoma hati ya mashtaka wakili wa Serikali Mwandamizi kutoka Takukuru, Vitalis Peter akisaidiana na Lilian William amedai Mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Salim Ally kuwa, mshtakiwa ametenda kosa hilo kati ya April Mosi mwaka 2011 na Julia 19, 2016 huko Katika Wilaya ya Ubungo mkoani Dar es Salaam.
Imedaiwa mshtakiwa akiwa ameajiriwa kama Afisa msaidizi wa forodha wa TRA alikutwa akimiliki Mali isiyolingana na Kipato chake ambapo, alikutwa anamiliki nyumba ya gorofa moja yenye thamani ya Sh. 698.921.217. kiwanja ambacho hakijasaliwa kilichopo eneo Mbezi Juu, Ubungo chenye thamani ya Sh. Milioni 7, Kiwanja kingine ambacho hakijasajiliwa chenye thamani ya Sh. 9.500.000 kilichopo eneo la Goba. Mali nyingine ni Kiwanja ambacho hakijasajiliwa chenye katika eneo la Kigamboni Wilayani Temeke chenye thamani ya Sh. Milioni 6.
Imedaiwa kuwa Mali yote hiyo ina thamani ya Sh. 721.421.217 mali ambayo hailingani na kipato chake cha sasa wala cha zamani. Hata hivyo mshtakiwa amekana kutenda kosa hilo na amerudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.
Mahakama Imemtaka mshtakiwa kuweka fedha taslimu Sh. 360.710.608 au kuweka mali isiyohamishika yenye thamani ya kiwango hicho cha fedha, Pia mshtakiwa ametakiwa kuwa na wadhamini wawili ambao kila mmoja anatakiwa kusaini bondi ya Milioni 360.
Aidha mshtakiwa ametakiwa kuwasilisha hati zake za kusafiri mahakamani hapo na Pia haruhusiwi kusafiri nje ya mkoa wa Dar es Salama bila ya kuwa na kibali.
Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo umeishakamilika na imeahirishwa hadi Januari 29,2018 kwa ajili ya mshtakiwa kuja kusomewa maelezo ya awali (PH) "
Aliyekuwa Afisa Msaidizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, (TRA) Godfrey Mapuga akipelekwa Katika chuma cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kusomewa tuhuma zake zinazomkabili za kumiliki mali ya zaidi ya Sh. Milioni 720. isiyolingana na kipato chake cha sasa wala cha zamani.
Aliyekuwa Afisa Msaidizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, (TRA) Godfrey Mapuga akipelekwa Katika chuma cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kusomewa tuhuma zake zinazomkabili za kumiliki mali ya zaidi ya Sh. Milioni 720. isiyolingana na kipato chake cha sasa wala cha zamani.
Hivyo makala Afisa msaidiazi wa TRA kizimbani kwa kumili mali zisizolingana na kipato chake
yaani makala yote Afisa msaidiazi wa TRA kizimbani kwa kumili mali zisizolingana na kipato chake Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Afisa msaidiazi wa TRA kizimbani kwa kumili mali zisizolingana na kipato chake mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/01/afisa-msaidiazi-wa-tra-kizimbani-kwa.html
0 Response to "Afisa msaidiazi wa TRA kizimbani kwa kumili mali zisizolingana na kipato chake"
Post a Comment