Loading...
title : AKINAMAMA WALIOJIFUNGUA 67 PAMOJA NA WATOTO WACHANGA 475 WAMEFARIKI MKOANI PWANI KUTOKANA NA UZAZI KATIKA KIPINDI CHA MWAKA 2018
link : AKINAMAMA WALIOJIFUNGUA 67 PAMOJA NA WATOTO WACHANGA 475 WAMEFARIKI MKOANI PWANI KUTOKANA NA UZAZI KATIKA KIPINDI CHA MWAKA 2018
AKINAMAMA WALIOJIFUNGUA 67 PAMOJA NA WATOTO WACHANGA 475 WAMEFARIKI MKOANI PWANI KUTOKANA NA UZAZI KATIKA KIPINDI CHA MWAKA 2018
NA MWAMVUA MWINYI, PWANI
JUMLA ya watoto wachanga 475 wamefariki dunia baada ya akinamama 41,064 kujifungua mkoani Pwani, mwaka 2018 ,hali ambayo inaonyesha idadi ya vifo vitokanavyo na uzazi kimkoa bado ipo juu. Aidha kati ya akinamama hao 41,064 waliojifungua akinamama 67 walifariki dunia kutokana na uzazi.
Hayo yalisemwa na mganga mkuu wa mkoa wa Pwani, dokta Gunini Kamba wakati mkuu wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo aliposaini hati ya makubaliano na wakuu wa wilaya ya kampeni ya kuzuia vifo vya uzazi, kampeni ambayo itafanyika kwa miezi 12 nchini. Alisema, vifo vya watoto wachanga na akinamama wanaojifungua hali hairidhishi hivyo kampeni hiyo itasaidia kupunguza idadi hiyo.
Kamba alisema, lengo hilo linaweza kufikiwa endapo akinamama watafuata maelekezo ya kiafya wanayopatiwa wakati wa uzazi ili waweze kuvuka salama katika kipindi cha uzazi. "Vifo 67 kwa waliojifungua na watoto wachanga 475 ukilinganisha na malengo ya Kitaifa bado hali sio nzuri sana "alisisitiza Kamba. Pamoja na hayo Kamba aliwataka ,akinamama wajawazito kuhakikisha wanaanza klinik ndani ya miezi 12 ya kwanza ili kujua afya zao.
Pia waendelee na kufuatilia afya zao kulingana na utaratibu watakaopatiwa hadi wakati wa kujifungua bila kupuuzia. "Na wakijifungua inapaswa kuhakikishwa ndani ya lisaa limoja baada ya kujifungua mtoto anyonye "alifafanua Kamba. Awali mkuu wa mkoa wa Pwani, Ndikilo aliwaasa wakuu wa wilaya kwenda kusimamia malengo hayo ili kufanikisha kampeni hiyo kiwilaya, mkoa na Taifa kijumla.
Hivyo makala AKINAMAMA WALIOJIFUNGUA 67 PAMOJA NA WATOTO WACHANGA 475 WAMEFARIKI MKOANI PWANI KUTOKANA NA UZAZI KATIKA KIPINDI CHA MWAKA 2018
yaani makala yote AKINAMAMA WALIOJIFUNGUA 67 PAMOJA NA WATOTO WACHANGA 475 WAMEFARIKI MKOANI PWANI KUTOKANA NA UZAZI KATIKA KIPINDI CHA MWAKA 2018 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala AKINAMAMA WALIOJIFUNGUA 67 PAMOJA NA WATOTO WACHANGA 475 WAMEFARIKI MKOANI PWANI KUTOKANA NA UZAZI KATIKA KIPINDI CHA MWAKA 2018 mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/01/akinamama-waliojifungua-67-pamoja-na.html
0 Response to "AKINAMAMA WALIOJIFUNGUA 67 PAMOJA NA WATOTO WACHANGA 475 WAMEFARIKI MKOANI PWANI KUTOKANA NA UZAZI KATIKA KIPINDI CHA MWAKA 2018"
Post a Comment