Loading...
title : ALIYEKUWA MKURUGENZI MKUU NIDA DICKSON MAIMU SASA AFUNGULIWA MASHTAKA 100,APANDISHWA KIZIMBANI
link : ALIYEKUWA MKURUGENZI MKUU NIDA DICKSON MAIMU SASA AFUNGULIWA MASHTAKA 100,APANDISHWA KIZIMBANI
ALIYEKUWA MKURUGENZI MKUU NIDA DICKSON MAIMU SASA AFUNGULIWA MASHTAKA 100,APANDISHWA KIZIMBANI
Na Karama Kenyunko globu ya Jamii,
BAADA ya kuachiwa huru na kukamatwa tena jana mchana, aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho (NIDA), Dickson Maimu na wenzake watano wamepandishwa katika kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashtaka 100 mapya yakiwemo mashtaka 25 ya utakatishaji fedha.
Wakili wa Serikali Wankyo Saimon akisaidiana na Wakili kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai amewataja washtakiwa wengine mbali na Maimu kuwa ni Meneja Biashara wa (NIDA), Aveln Momburi,
Mkurugenzi wa Kampuni ya Aste Insurance Brokers, Astery Ndege, Ofisa Usafirishaji, George Ntalima, Mkurugenzi wa Sheria, Sabina Raymond na Xavery Kayombo.
Katika mashtaka hayo ambayo yamesomwa mbele ya Hakimu Mkazi Salum Ally, washtakiwa wanakabiliw Na mashtaka 22 ya kughushi, mashtaka 43 ya kutumia nyaraka kwa lengo la kumdanganya mwajiri, mashtaka mawili ya kula njama, mashtaka 25 ya kutakatisha fedha na mashtaka matano ya kuisababishia hasara NIDA.
Pia washtakiwa wanakabiliwa Na mashtaka mawili ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na shtaka moja la matumizi mabaya ya madara lipo moja ambalo linamkabili Maimu na Sabina.
Katika shtaka la kwanza la kula njama Maimu, Ndege na Ntalima wanadaiwa, kati ya Julai 19, 2011 na Agosti 31,2015 wakiwa maeneo tofauti tofauti ndani ya Jiji la Dar es Salaam walikula njama ya kufanya udanganyifu wa Sh bilioni 1.175 dhidi ya NIDA.
Pia Maimu anatuhumiwa kutakatisha fedha kiasi cha sh bilioni 1,175,785,600.93 kati Julai 19,2011 na Agosti 31, 2015 ambapo anadaiwa kujihusisha moja kwa moja kuhamisha fedha hizo huku akijua ni zao la kosa la kughushi.

Katika shtaka jingine, Maimu na Raymond wanatuhumiwa November 7, 2011 wakiwa Makao Makuu ya NIDA, Kinondoni jijini Dar es Salama walitumia madaraka yao vibaya na kusababisha huo cha sheria (Law School) Dar es Salaam na Kampuni ya Gotham International Ltd kupata faida ya Sh .899,935,494.
Imedaiwa kati ya Novemba 12, 2011 na Mei 12, 2015, Maimu na Momburi wakiwa makao makuu ya NIDA, Kinondoni akiwa Mkurugenzi na Meneja wa biashara walishindwa kusimamia ujenzi wa jengo lililopo plonti namba 39A na kuikuisababishia mamlaka hiyo hasara ya Sh 402,210,885.02.
Aidha imeendelea kudaiwa kuwa kati ya Julai 19,2011 na Agosti 12, 2011, washtakiwa Maimu na Ntalima wakiwa Makao Makuu ya NIDA walitumia nyaraka ya uongo kwa nia ya kumdanganya mwajiri wao kuwa walitumia stakabadhi ya malipo namba 0034 na namba 0035 kuilipa Kampuni ya Aste Insurance Brokers Ltd dola za Marekani 10,300.00.
Hata hivyo, washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama ya Kisutu haina Mamlaka ya kusikiliza kesi za Uhujumu uchumi, hadi Mahakama Kuu kwa kupata kibali kutoka kwa DPP.
Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo umeshakamilika na tayari wamewasalisha maelezo ya mashahidi Mahakama Kuu.
Katika kesi hiyo washtakiwa, Momburi na Raymond wao hawajapatikana na kosa la kutakatisha fedha, kwa hiyo mashtaka yao yanadhaminika, hivyo upande wa utetezi uliiomba mahakama kuwapatia washtakiwa hao dhamana.
upande wa mashtaka ulieleza kuwa dhamana iko wazi kwa washtakiwa hao, lakini si hapa ni Mahakama Kuu kama wanataka wanaweza kupeleka maombi ya dhamana Mahakama Kuu.
"Njia pekee ni wapeleke maombi yao Mahakama Kuu yakasikilizwe na kutolewa uamuzi kwa sababu sisi hatuna Mamlaka ya kusikiliza kesi hii," amsema hakimu Ally
Kesi hiyo imeahirishwa hadi February 12 mwaka huu, ambapo washtakiwa watasomewa maelezo ya mashahidi (Committal)
Hivyo makala ALIYEKUWA MKURUGENZI MKUU NIDA DICKSON MAIMU SASA AFUNGULIWA MASHTAKA 100,APANDISHWA KIZIMBANI
yaani makala yote ALIYEKUWA MKURUGENZI MKUU NIDA DICKSON MAIMU SASA AFUNGULIWA MASHTAKA 100,APANDISHWA KIZIMBANI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala ALIYEKUWA MKURUGENZI MKUU NIDA DICKSON MAIMU SASA AFUNGULIWA MASHTAKA 100,APANDISHWA KIZIMBANI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/01/aliyekuwa-mkurugenzi-mkuu-nida-dickson.html
0 Response to "ALIYEKUWA MKURUGENZI MKUU NIDA DICKSON MAIMU SASA AFUNGULIWA MASHTAKA 100,APANDISHWA KIZIMBANI"
Post a Comment