Loading...

BANK YA DUNIA KUENDELEA KUIPA TANZANIA MIKOPO YA GHARAMA NAFUU

Loading...
BANK YA DUNIA KUENDELEA KUIPA TANZANIA MIKOPO YA GHARAMA NAFUU - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa BANK YA DUNIA KUENDELEA KUIPA TANZANIA MIKOPO YA GHARAMA NAFUU, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : BANK YA DUNIA KUENDELEA KUIPA TANZANIA MIKOPO YA GHARAMA NAFUU
link : BANK YA DUNIA KUENDELEA KUIPA TANZANIA MIKOPO YA GHARAMA NAFUU

soma pia


BANK YA DUNIA KUENDELEA KUIPA TANZANIA MIKOPO YA GHARAMA NAFUU

Mwakilishi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Bi. Bella Bird amemhakikishia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuwa benki hiyo imejipanga kuendelea kutoa mikopo nafuu kwa miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini ili kukuza uchumi na kupunguza umasikini.

Bi. Bella Bird ametoa kauli hiyo leo tarehe 04 Desemba, 2017 Ikulu Jijini Dar es Salaam na kubainisha maeneo ya kipaumbele kuwa ni miundombinu hususani barabara na reli, kuongeza uzalishaji na usambazaji wa nishati ya umeme, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na elimu kwa kujielekeza katika ubora na kuhakikisha idadi ya wanaopata elimu inaongezeka.

Maeneo mengine ni kuboresha sekta ya afya, kuongeza upatikanaji wa maji, usimamizi bora wa ardhi, mawasiliano, huduma za fedha jumuishi, vituo vya pamoja vya Serikali na kusaidia familia masikini.

Bi. Bella Bird amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Benki ya Dunia na amemuahidi kuwa benki hiyo itaendelea kushirikiana kwa karibu na Tanzania katika utekelezaji wa miradi mingine.

“Mwaka uliopita Benki ya Dunia imetoa mikopo nafuu yenye thamani ya Dola za Marekani Bilioni 1.2 (Shilingi Trilioni 2.7) kwa Tanzania, fedha hizi zimekwenda katika miradi mbalimbali na tunafurahi kuwa miradi hiyo inakwenda vizuri na wananchi wanafurahia, kwa sasa tunapanga namna tutakavyotoa mikopo kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za maendeleo katika kipindi kijacho” amesema Bi. Bella Bird.

Kwa upande wake Mhe. Rais Magufuli ameishukuru Benki ya Dunia kwa ushirikiano wake na Tanzania katika maendeleo na amemhakikishia Bi. Bella Bird kuwa Serikali itazisimamia vizuri fedha zote zinazotolewa na benki hiyo ili zilete matokeo yanayotarajiwa.

Mhe. Rais Magufuli ameongeza kuwa maeneo yote ambayo benki hiyo imeyataja kuwa kipaumbele katika fedha zitakazotolewa kuanzia sasa ni muhimu kwa ustawi wa Tanzania na amesisitiza kuwa fedha zitakazotolewa kwa mkopo zielekezwe katika maendeleo na sio vinginevyo.

“Naishukuru sana Benki ya Dunia kwa kutuunga mkono, nitafurahi kuona mnaendelea kutupatia fedha ambazo zinaelekezwa kwenye miradi ya maendeleo na kuleta manufaa mapana na endelevu, badala ya kugawa fedha kwa watu na baadaye nchi inakuja kuzilipa kwa kukusanya kodi za wananchi” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli leo ameongoza kikao cha Baraza la Mawaziri Kilichofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.
 
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
04 Desemba, 2017


Hivyo makala BANK YA DUNIA KUENDELEA KUIPA TANZANIA MIKOPO YA GHARAMA NAFUU

yaani makala yote BANK YA DUNIA KUENDELEA KUIPA TANZANIA MIKOPO YA GHARAMA NAFUU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala BANK YA DUNIA KUENDELEA KUIPA TANZANIA MIKOPO YA GHARAMA NAFUU mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/12/bank-ya-dunia-kuendelea-kuipa-tanzania.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "BANK YA DUNIA KUENDELEA KUIPA TANZANIA MIKOPO YA GHARAMA NAFUU"

Post a Comment

Loading...