Loading...

Felix Tshisekedi: Mgombea wa upinzani ashinda uchaguzi wa urais DRC

Loading...
Felix Tshisekedi: Mgombea wa upinzani ashinda uchaguzi wa urais DRC - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Felix Tshisekedi: Mgombea wa upinzani ashinda uchaguzi wa urais DRC, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Felix Tshisekedi: Mgombea wa upinzani ashinda uchaguzi wa urais DRC
link : Felix Tshisekedi: Mgombea wa upinzani ashinda uchaguzi wa urais DRC

soma pia


Felix Tshisekedi: Mgombea wa upinzani ashinda uchaguzi wa urais DRC

Wafuasi wa Felix Tshisekedi awali walikusanyika nje ya makao makuu ya chama chake Limete, Kinshasa Jumatano


Felix Tshisekedi ameshinda uchaguzi wa urais nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, tume ya uchaguzi imesema.

Matokeo ya awali yanaonyesha mgombea huyo wa upinzani amemshinda mgombea mwingine wa upinzani Martin Fayulu, pamoja na mgombea aliyekuwa anaungwa mkono na serikali Emmanuel Shadary.

Mkuu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Ceni) Corneille Nangaa, alisema mapema Alhamisi kwamba Bw Tshisekedi alipata asilimia 38.57 ya kura zilizopigwa na "anatangazwa mshindi wa urais mteule."

Tshisekedi alipata zaidi ya kura 7 milioni naye bw Fayulu akapata kura takriban 6.4 milioni, huku mgombea wa serikali Emmanuel Ramazani Shadary akipata takriban kura 4.4 milioni.

Iwapo matokeo hayo yatathibitishwa, Bw Tshisekedi atakuwa mgombea wa kwanza kabisa wa upinzani kushinda uchaguzi wa urais tangu DRC ilipojipatia uhuru.

Bw Tshisekedi yuko kwenye muungano wa kisiasa aliyekuwa mgombea wa chama cha UNC (Union for the Congolese Nation) Vital Kamerhe UNC ambapo walikuwa wamekubaliana kwamba Tshiskedi atagombea wadhifa wa rais naye Kamerhe awe waziri mkuu iwapo muungano wao utashinda urais.

Rais Joseph Kabila anatarajiwa kuondoka madarakani baada ya kuongoza kwa miaka 18.Mgombea wake aliyemteua kuwakilisha muungano tawala Emmanuel Ramazani Shadary amemaliza wa tatu.

Martin Fayulu ambaye awali alikuwa mgombea wa pamoja wa muungano wa upinzani kabla ya Tshisekedi na mgombea wa chama cha UNC (Union for the Congolese Nation) Vital Kamerhe kujiondoa kutoka kwenye muungano huo na kuunda muungano wao wawili, alimaliza akiwa nafasi ya pili.



Hivyo makala Felix Tshisekedi: Mgombea wa upinzani ashinda uchaguzi wa urais DRC

yaani makala yote Felix Tshisekedi: Mgombea wa upinzani ashinda uchaguzi wa urais DRC Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Felix Tshisekedi: Mgombea wa upinzani ashinda uchaguzi wa urais DRC mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/01/felix-tshisekedi-mgombea-wa-upinzani.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Felix Tshisekedi: Mgombea wa upinzani ashinda uchaguzi wa urais DRC"

Post a Comment

Loading...