Loading...

KITWANA MANARA: MWANASOKA HODARI ALIYEKUWA NA VIPAJI VYA AJABU NA REKODI ZA KIPEKEE TZ!!!

Loading...
KITWANA MANARA: MWANASOKA HODARI ALIYEKUWA NA VIPAJI VYA AJABU NA REKODI ZA KIPEKEE TZ!!! - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa KITWANA MANARA: MWANASOKA HODARI ALIYEKUWA NA VIPAJI VYA AJABU NA REKODI ZA KIPEKEE TZ!!!, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : KITWANA MANARA: MWANASOKA HODARI ALIYEKUWA NA VIPAJI VYA AJABU NA REKODI ZA KIPEKEE TZ!!!
link : KITWANA MANARA: MWANASOKA HODARI ALIYEKUWA NA VIPAJI VYA AJABU NA REKODI ZA KIPEKEE TZ!!!

soma pia


KITWANA MANARA: MWANASOKA HODARI ALIYEKUWA NA VIPAJI VYA AJABU NA REKODI ZA KIPEKEE TZ!!!

1. Usuli:

Ijumaa jioni ya 5.5.1941 huko Kigoma, Mwenyezi Mungu aliwajaalia Bw RAMADHAN MANARA na Bi. MISHI MIKESSY mtoto wa kiume waliyempa jina la KITWANA. Mtoto huyo aliyezaliwa na vipaji vya ajabu na vya kipekee kuliko wanasoka wote Tanzania, alikuwa ni mtoto wa 2 kati ya watoto 6 wa wazee hao.

KITWANA alianza kupenda mpira alipokuwa shule ya msingi Mchikichini, baada ya kuhamia Dar es salaam. Akiwa shuleni hapo, KITWANA alikuwa maarufu tangia akiwa madarasa ya chini kwani alikuwa na vipaji vikubwa vya soka tofauti na watoto wenzie kwani alikuwa akicheza nafasi mbalimbali ingawa  alin'gara zaidi kwenye ukipa.

Baada ya kumaliza shule na kuanza kuchezea timu za mtaani, KITWANA alikuwa akipenda sana kupiga msosi wa uhakika na "kujifua" baharini peke yake kama mwehu!. Wahindi waliokuwa wakimuona mara kwa mara walikuwa wakimshangaa na kupelekea kumbatiza jina la Kihindi "POPAT" yaani "Mtu Fyatu"!.
 2. Kuchezea Timu Kubwa:

KITWANA, kutokana na uhodari wake,  mwaka 1960 alijiunga na Cosmopolitans ambayo ilikuwa maarufu sana enzi hizo na kuwa kipa wake wa kwanza na baadae akachaguliwa kuwa kipa wa timu ya Taifa ya Tanganyika.

Mwaka 1962, KITWANA akachukuliwa na timu ya TPC ya Moshi iliyokuwa timu tajiri kuliko zote nchini iliyosajili nyota wote wa wakati huo. Baada ya uhodari wake kusambaa, KITWANA alichukuliwa na timu ya Feisal FC ya Mombasa ya ligi kuu ya Kenya na kuwa mchezaji wa kulipwa.

KITWANA akiwa na wenzake timu ya taifa ya Tanganyika waliweza kutwaa kombe la Gossage lilipofanyika uwanja wa Karume, Dar es salaam mwaka 1965 na Rais JULIUS K. NYERERE aliwapongeza sana kwa kuliletea taifa heshma kubwa.

KITWANA akaenda Kenya kuendelea na timu yake ya Feisal FC.

KITWANA aliporudi likizo nchini, bibi yake, SALMA BINTI JUMA, aliyekuwa mpenzi kindakindaki wa Yanga alimuweka kitako na kumueleza kuwa wazee wa Yanga wamesema "piga ua, garagaza" ni lazma KITWANA achezee Yanga. Bila hiana, KITWANA akawa si tu mchezaji bali pia mwanachama wa timu hiyo msimu wa 1965/66.
3. YANGA vs Taifa Stars:

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, katika timu ya YANGA, KITWANA alikuwa mshambuliaji mahiri akivaa jezi na.9, lakini akiwa timu ya Taifa alikuwa kipa "Tanzania One"!.

Watu wengi walikuwa hawaelewi ni kwa vipi mchezaji akawa na vipaji hivyo vikubwa kiasi hicho cha kucheza nafasi inayohitaji mikono na nyingine miguu.! KITWANA alikuwa mchezaji mrefu sana, mwenye misuli minene na mwepesi sana kuruka na hodari mno kwa magoli ya vichwa. Ilikuwa ni bora timu ipambanayo na Yanga ipigiwe penati kuliko kona! Ilikuwa kawaida ABRAHMAN JUMA akipiga kona, KITWANA kuingia wavuni yeye, mpira na mabeki hata wanne kwani ilikuwa vigumu mno kumkabili kutokana na umbile lake, maguvu yake na uwezo usio wa kawaida wa kuruka!.

4. YANGA kutamba Barani Afrika 1969 & 1970;

KITWANA aliisaidia sana YANGA kutwaa ubingwa nchini na kisha kuiwezesha YANGA kuwa TIMU YA KWANZA Tanzania kufika robo fainali ya Klabu Bingwa ya Afrika kwani ilifanya hivyo mwaka 1969. Engineer HAJI MANARA soooma hii historiiaaa!!! 

Katika robo fainali, YANGA ilipangiwa timu kali ya ASANTE KOTOKO ya Ghana. Mechi ya kwanza ilichezwa Kumasi, Ghana na ikaisha kwa sare ya 1-1. Kipute cha marudiano kikapigwa "Shamba la Bibi" Dar es salaam, na matokeo yakawa 1-1 tena hivyo timu hizo zikawa sare 2-2. Enzi hizo sheria ya mikwaju ya penati haikuwepo.
Ikabidi irushwe shilingi ambapo nahodha wa Yanga, ABRAMAN JUMA 'aliingizwa mjini' na nahodha wa Kotoko. Refa alipoirusha tu shilingi na kabla haijadondoka kujua mshindi ni nani, nahodha wa Kotoko nae akaruka juu na kumkumbatia refa na kumpa mkono kana kwamba shilingi hio imeishadondoka na mshindi kujulikana! Refa mwenyewe alichanganyikiwa na JUMA nae alichanhanyikiwa na hakujua kinachoendelea akabaki kashika tama na ndio ukawa mwisho wa Yanga michuano hiyo.!

Mwaka 1970, YANGA iliingia tena robo fainali na ikapangiwa tena miamba hiyo ya Ghana iliyokuwa ikiogopwa bara zima la Afrika. Kotoko ilikuwa na kipa bora kuliko wote Afrika aliyeitwa MENSAH aliyepelekea washabiki wa Yanga wampe jina hilo kipa wao wa baadae JUMA PONDAMALI.

Yanga ilikwenda Romania kujifua chini ya kocha PETER MANDAWA kabla ya kukutana na ASANTE KOTOKO. Miamba hiyo miwili, kwa mara nyingine, ikatoshana nguvu. Mechi ya Kumasi na ya Dar es salaam zote zikaishia kwa sare. YANGA hawakutaka tena kuskia "hadithi za Esopo" za kurusha shilingi. Ikabidi kipute kipigwe "neutral ground" huko Ethiopia. Huko, Yanga ikafungwa 2-0 safari hii za halali kabisa kwani MENSAH alifanya vitu visivyo vya kawaida golini kwa kuokoa michomo 3 akiwa ana kwa na KITWANA!. Yanga ikafa kiume.

5. SIMBA Kugoma Kutia Timu kwa Kuogopa "Muziki" wa YANGA!!!

Tarehe 1.6.1968 ilikiwa ni siku ya kipekee kwa historia ya YANGA. Siku hiyo ilikuwa ya kukabidhiwa jengo lake na siku ya kupambana na mtani wake, SUNDERLAND(Simba).

Siku hiyo, kabumbu lililopigwa na YANGA, iliyokuwa ikiogopewa ukanda wote huu, "lilikuwa si la nchi hii'. Mnyama SIMBA alikula bao 5-0 kama amesimama. SIMBA walikuwa wakimuogopa sana KITWANA hivyo mabeki wote walimlinda yeye tu na matokeo yake mabao 4 yakafungwa na wachezaji wengine huku KITWANA 'akisukumia ndani' bao la 5 dk ya 85. Baada ya bao hilo, wachezajibwa YANGA hawakutaka kuongeza magoli bali walianza kuwakoga SIMBA kwa kupiga kanzu, vyenga vya mauzi na pasi murua. Hii ikawaondosha uwanjani wapenzi wa SIMBA huku timu yao ikiwa imeloa chapachapa !!! 

Mechi ya ligi  baina ya watani hao, mwaka uliofuata, ikapangwa kuchezwa tarehe 3.3.1969. Mnyama SIMBA akiwa bado anaukumbuka "Mziki" wa 5-0, na huku YANGA ikiwa katika kiwango bora kabisa, aliona kuna kila dalili zingekuwa si chini ya bao 10-0 hivyo akaona "kama mbwai, mbwai tu. Bora lawama kuliko fedheha" na akaona heri kupigwa faini kuliko kuchezea kichapo cha mbwa koko!. SIMBA ikapigwa faini na YANGA kupewa pointi 2 na magoli 2.

KITWANA akaendelea kuiletea YANGA mafanikio lukuki ambapo kwa miaka 5 mfululizo kati ya 1968-1973, SIMBA iliusikia ubingwa redioni tu! Mwaka 1975, YANGA ikatwaa ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati baada ya kumtandika Mnyama SIMBA bao 2-0 swaaafi pale Zanzibar.

6. KITWANA kuzitosa Yanga na Taifa Stars:


Baada ya mgogoro mkubwa uliofumuka klabuni YANGA,  KITWANA na wachezaji hodari wa Yanga wakaitosa timu hiyo.


Aidha, mwaka 1976, KITWANA alistaafu kuchezea timu ya Taifa.

7. Vipaji Kuntu na Rekodi Mujarab za KITWANA:

7.1 KITWANA ndiye alikuwa kipa wa Kwanza wa Tanganyika "Tanganyika One".

7.2 KITWANA ndiye mchezaji pekee aliyekuwa akicheza kama Kipa na Mshambuliaji katika timu 2 tofauti.

7.3 KITWANA alikuwa mpiga vichwa hodari kuliko mchezaji yeyote aliyepata kutokea Tanzania (M. KIKWA, A. SABU, A. MZIBA na Babu MEDI KAGERE wote hao wanasubiri saaana).

7.3 KITWANA ndiye mfungaji wa magoli mengi kwenye ligi katika historia ya kabumbu nchini akifuatiwa kwa mbaali na MOHAMED HUSSEIN "MMACHINGA".

7:4 KITWANA ndiye mchezaji aliyeichezea timu ya Taifa kwa miaka mingi kuliko wote (1960-1976).

7.5 KITWANA ndiye mchezaji wa kwanza nchini kwenda nje kucheza mpira wa kulipwa (Kenya).

7.6 KITWANA anatoka FAMILIA BORA KULIKO ZOTE ZA KANDANDA TZ ( SUNDAY & KASSIM-wote wameichezea Yanga na Taifa Stars kwa mafanikio makubwa).

7.8 KITWANA ni mmoja wa wachezaji WATATU TU ambao wameweza kufunga magoli katika mechi 3 mfululizo za watani, SIMBA na YANGA. Wengine ni AMIS TAMBWE na MADARAKA SULEIMAN "Mzee wa Kiminyio".

7.9 Tarehe 3.6.2015, katika kuadhimisha miaka 50 ya FIFA  ukumbi wa JB Belmonte, Dar es salaam, KITWANA alizawadiwa Medali Maalumu kwa mchango wake mkubwa katika soka nchini.

7.10 Ijumaa, tarehe 26.5.2017, TFF ilimzawadia KITWANA TUZO YA MCHEZAJI BORA KULIKO WOTE WA ZAMANI katika hafla iliyofanyika Mlimani City kuzawadia wanasoka mbalimbali.

8. Maisha Baada ya Kustaafu Soka:

KITWANA ni mmoja wa wanasoka wachache wenye maisha mazuri Tanzania akiishi Baracuda Tabata. Aliwahi kuwa Diwani wa CCM Buguruni na pia amewahi kuhudumu kwenye Kamati mbalimbali za FAT/TFF.

Kwa hakika, KITWANA RAMADHANI MANARA "POPAT", ni mchezaji aliyekuwa na vipaji visivyo vya kawaida ambavyo havijawahi lutokea nchini na mwenye kujituma sana kwenye mazoezi binafsi!.

Tafakuri Tunduizu:

Je, ni kwanini wachezaji wa siku hizi ni wavivu sana? Ni kwanini wachezaji hawa humchukia kocha awapae mazoezi magumi na kumuundia zengwe atimuliwe? Kwanini hawapendi mazoezi binafsi? Kwanini wanapenda sana kushindia_chips zege_ ?


Hivyo makala KITWANA MANARA: MWANASOKA HODARI ALIYEKUWA NA VIPAJI VYA AJABU NA REKODI ZA KIPEKEE TZ!!!

yaani makala yote KITWANA MANARA: MWANASOKA HODARI ALIYEKUWA NA VIPAJI VYA AJABU NA REKODI ZA KIPEKEE TZ!!! Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala KITWANA MANARA: MWANASOKA HODARI ALIYEKUWA NA VIPAJI VYA AJABU NA REKODI ZA KIPEKEE TZ!!! mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/01/kitwana-manara-mwanasoka-hodari.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "KITWANA MANARA: MWANASOKA HODARI ALIYEKUWA NA VIPAJI VYA AJABU NA REKODI ZA KIPEKEE TZ!!!"

Post a Comment

Loading...