Loading...
title : MAFANIKIO YA TAGOANE YAFUNGUA NJIA KWA WASANII WA INJILI
link : MAFANIKIO YA TAGOANE YAFUNGUA NJIA KWA WASANII WA INJILI
MAFANIKIO YA TAGOANE YAFUNGUA NJIA KWA WASANII WA INJILI
Rais wa mtandao wa wasanii wa Injili na Maadili Dkt. Godwin Maimu akizungumza katika Tamasha hilo lililofanyika Buza Jijini Dar es salaam Buza Kipera
Picha ya Viongozi wa Mtandao wa wasanii wa Injili na maadili wa pili kutoka kulua ni Rais wa Tagoane Taifa Dkt. Godwin Maimu, aliyrpo kushoto kwake ni Katibu mkuu Mchungaji Lucy, wa kwanza kushoto ni Katibu mkuu mwenza Silvanus Mumba akifuatiwa na Makamu wa Rais Tagoane, Florah Sungura.
Mchungaji mwenyeji Tamasha lilipofanyika Apostal Israel Popapo kutoka Jijini Dar es salaam, katika kanisa la ETERNITY GOSPEL CHURCH, Buza Kipera
Uimbaji ukiendelea kama inavyoonekana katika picha kafika kanisa la ETERNITY GOSPEL CHURCH Buza Kipera
Picha ya pamoja ya wasanii mbalimbali wa Injili waluohudhuria katika tamadha hilo lililopewa jina la Madhabahu ya shukrani
NA.VERO IGNATUS
Mtandao wa wasanii wa Injili na maadili Nchini(Tagoane) wanafanya Tamasha leo la kutoa shukrani kwa Mungu kwa kuwapa ulinzi na Kibali tangia kuanzishiswa kwa mtandao huo
Akizungumza katibu mkuu mtendaji Tagoane Taifa Silvanus Mumba amesema kuwa Tamasha hilo wamelipa jina la Tukuza Festival Madhabahu ya shukrani ambapo wananzia Jijini Dar es salaam ndipo wataelekea mikoa mingine
Amesema lengo kuu ni kumshukuru Mungu kwa matendo makuu aliyowatendea tangia kuanzishwa kwa mtandao huo sambamba na mafanikio yaliyopatikana ya kuwaleta waimbaji wa pamoja.
Silvanus amesema kuwa hadi sasa wamekuwa na Mafanikio Makubwa tangia kuanzishwa kwa TAGOANE, wameweza kusaidia Watoto Yatima, wameutangaza Utalii wa ndani wameweza kusaidia Vifaa vya matibabu katika Hospitali Mount Meru sambamba na kusaidia Vijana Elimu juu ya ujasiliamali,
Akielezea matazamio waliyonayo ni kuweza kuwasaidia wasanii Kuwa na UCHUMI imara kupitia Mfuko wa TAGOANE LOAN FUND, Kuwa na Wasanii walio Tayari kujito kwaajili ya Jamii na makundi Maalumu Kama Wazee, Yatima, wajane, vilema, na Wagonjwa
Amesema kuwa wanaendelea Kuwa na Utaratibu wa Kuibua vipaji Mashuleni kwa Kushirikiana na Taasisi ya waalimu wa shule BinafsiTanzania (TPTU) Lakini pia Kujiunganisha na wadau wa Maendeleo Kama SIHAONE TUNAPENDANA Ltd
Tunapenda kuwaambia Wasanii wote, wakristo walio Kwenye sekta ya Sana, kujiunga na TAGOANE kwasababu ndio Pahala sahihi amvako wataweza kujiweka Akiba na kukopa inapohitajika, Kupata Fursa ya Mafunzo ya ujasiliamali na Sheria ya hatimiliki, Elimu juu ya Ubunifu Lakini pia Watajitolea kwa jamii pia ifaidike kupitia yeye
Mikoa mingine ambayo wanatazamia kufanya Tamasha hilo ni pamoja na Dodoma, Morogoro, kwa sasa wameanza na Jiji la Dar es salaam mikoa mingine wataendelea kutoa taarifa , lengo kuu ni Kumpelekea Mungu Shukurani za pekee kwa Kuisimamisha Tagoane Kuwa ya Mfano.
Hivyo makala MAFANIKIO YA TAGOANE YAFUNGUA NJIA KWA WASANII WA INJILI
yaani makala yote MAFANIKIO YA TAGOANE YAFUNGUA NJIA KWA WASANII WA INJILI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAFANIKIO YA TAGOANE YAFUNGUA NJIA KWA WASANII WA INJILI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/01/mafanikio-ya-tagoane-yafungua-njia-kwa.html
0 Response to "MAFANIKIO YA TAGOANE YAFUNGUA NJIA KWA WASANII WA INJILI"
Post a Comment